Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ilichukua saa nzima baada ya ajali hiyo mbaya ajali hiyo kuripotiwa ambayo imeua wanamaji saba waliokuwa katika manuari nje ya pwani ya Japan.
Maafisa kutoka nchi zote mbili wamesema kuwa ajali hiyo iliripotiwa na meli zote mbili takriban saa 2.30am Jumamosi, lakini takwimu za ufuatiliaji zinaonyesha kuwa ajali ilitokea saa 1:30am.
Ufuatiliaji huo wa data unaonyesha meli ya mizigo ikigeuka kipindi kifupi baada ya saa 1:30 na kurejea pale ilipokuwa muda wa saa 1:30.
Msemaji wa manuari za Marekani amesema inavyoelekea ajali ilitokea muda wa saa !:30am Jumamosi, na sio saa 2:30 am kama ilivyoripotiwa na manuari ya USS Fitzgerald.
Nanami Meguro, msemaji wa Nippo Yusen, msimamizi wa meli hiyo ya mizigo amesema taarifa za ufuatiliaji wa meli zinaonyesha kuwa meli ilikuwa “inafanya kazi kama kawaida” mpaka pale ajali ilipotokea saa 1:30 am. Lakini hakuwa na taarifa yoyote kuhusu ucheleweshaji wa ripoti ya ajali.
“Kwa sababu ilikuwa ni hali ya dharura, wafanyakazi wa meli inawezekana hawakuweza kutoa taarifa kwa haraka,” amesema.
Ajali hiyo inachunguzwa na Jeshi la majini la Marekani na Jeshi la majini la Japan ikishirikiana na bodi ya usalama ya usafirishaji ya Japan.
Mapema Jumatatu, Jeshi la Majini la Marekani liliwatambua wanamaji wake saba ambao walikutwa wamekufa katika vyumba vya kulala vilivyokuwa vimefurika maji.