Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 23:59

Wanamaji wa Marekani wa manuari ya Fitzgerald wakutwa wamekufa


Meli ya mizigo iliyogongana na manuari ya jeshi la marekani nje ya pwani ya Japan.
Meli ya mizigo iliyogongana na manuari ya jeshi la marekani nje ya pwani ya Japan.

Jeshi la majini la Marekani limesema kuwa wapiga mbizi wake wameweza kufika katika chumba cha manuari yake ya Fitzgerald kilichokuwa kimefurika maji na kugundua baadhi ya miili ya wahanga wa ajali hiyo.

Wanamaji wake walitoweka baada ya manuari hiyo ya kivita kugongana na meli ya mizigo, lakini juhudi za kuwatafuta zilizaa matunda pamoja na hali ngumu iliyowakabili.

Naibu Admiral Joseph Aucoin, ambaye ni kamanda wa Manuari hiyo namba 7, amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika kituo cha kijeshi cha Yokosuka Jumapili.

Hata hivyo alisita kusema ni miili mingapi iliokuwa imepatikana, lakini harakati za kutafuta waliotoweka zimesitishwa, amesema.

Majina ya wanamaji hao waliopoteza maisha katika ajali ya manuari hiyo yamehifadhiwa, mpaka pale familia zao zitakapopewa taarifa.

Manuari hiyo iligongana mapema Jumamosi na ile ya meli ya mizigo inayoitwa ACX Crystal- meli ambayo ukubwa wake ni mara nne ya ukubwa wa manuari ya kivita—iliyokuwa nje kabisa ya pwani ya Japan. Meli hiyo ya Ufilipino yenye tani 29,000 ina urefu wa mita 222, wakati manuari ya kivita ina uzito wa tani 8,315 na urefu wa mita 154.

“Uharibifu uliotokea katika ajali hiyo ni mkubwa. Kulikuwa na mpasuko mkubwa chini ya maji,” amesema Aucoin. Juhudi za kudhibiti uharibifu uliokuwa unakatisha tamaa zilizochukuliwa na wafanyakazi wa meli ziliwezesha kuikoa meli hiyo, amesema.

XS
SM
MD
LG