Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:04

Mawakili, wachunguzi waungana na Mueller kuchunguza Russia, Trump


Robert Mueller
Robert Mueller

Moja kati ya walioajiriwa aliwafuatilia magaidi katika miaka ya 90 kwa ajili ya FBI na baadae alisaidia kufungua kesi ya jinai dhidi ya mshukiwa wa tukio la kigaidi la 9/11 aliyejulikana kwa jina la Zacarias Moussaoui.

Mwendesha mashtaka mwengine ni yule aliongoza kikundi maalum cha uchunguzi cha serikali kuu kilichofuatilia kashfa ya Shirika la Enron katika mwaka 2000.

Watatu amesimamia utetezi wa kesi zaidi ya 100 za jinai mbele ya Mahakama Kuu akiwa katika nafasi ya naibu mtetezi mkuu kwenye Idara ya Sheria

Hawa ni kati ya wanasheria wenye uwezo mkubwa wa timu ya Mwendesha mashtaka Maalum Robert Mueller ambaye ameajiriwa hivi karibuni kuchunguza kuingilia kati kwa Russia katika uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka jana.

Na pia kuchimbua iwapo kulikuwa na ushirikiano wowote kati ya Moscow na timu ya Kampeni ya Donald Trump kabla hajachaguliwa kuwa rais Novemba.

Kwa kifupi, Mueller amewaajiri wanasheria 13 tangu alipoteuliwa mwezi mmoja uliopita, na anatarajia kuongeza wengine kadhaa, amesema msemaji wake, Peter Carr.

Uchunguzi huo, amesema Peter Zeidenberg, ambaye aliwahi kutumikia kama msaidizi maalum wa upande wa utetezi mwaka 2005 kufuatia uchunguzi wa aliyekuwa msaidizi wa ikulu ya White House, Scooter Libby, inaweza ikawahusisha dazeni ya wafanyakazi wa FBI na idadi kubwa ya waendesha mashtaka.”

Ajira za watu wenye uwezo mkubwa zimezingatia kuajiri wanasheria wenye weledi wa hali ya juu. Linaonyesha jinsi Mueller alivyochukua hatua makini katika uchunguzi huu, baada ya kukabidhiwa shughuli hii Mei 17, siku nane baada ya Rais Trump kumfukuza kazi Mkurugenzi wa FBI James Comey.

Trump amerejea kusema kuwa uchunguzi huo sio sahihi na kusema ni hatua ya “kumtafuta mchawi,” na kutangaza kuwa “hakuna mtu ambaye amekuja na ushahidi” kuwa yeye au timu ya kampeni yake walihusika na vitendo vyovyote kinyume cha sheria wakishirikiana na maafisa wa Russia.

Siku ya Alhamisi, rais aliishambulia timu ya Mueller, akisema kuwa uchunguzi huu “unaongozwa na baadhi ya watu ambao ni wabaya na wenye maslahi binafsi” – akikusudia kwamba kuna taarifa baadhi ya watu walioajiriwa na Mueller wametoa michango siku za nyuma kwa wagombea wa chama cha Demokrati wakati wa kampeni zao za kisiasa.

XS
SM
MD
LG