Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 08:38

Trump ashambulia uchunguzi unaofanywa na Mueller


Rais Donald Trump na Kushner

Mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller anachunguza iwapo Rais Donald Trump alizuia sheria kufuata mkondo wake.

Mapema Alhamisi, Trump aliingia katika safu anayoipenda ya mitandao ya jamii na kushambulia ripoti zilizoelezea kuwa mwendesha mashtaka maalum anachunguza madai ya kuwa rais aliingilia kati uchunguzi uliokuwa unafanyika dhidi yake.

“Walifanya majumuisho ya uongo kuhusiana na taarifa ya Russia, hawakukuta ushahidi wowote, na sasa wananituhumu kwa kuzuia sheria kufuata mkondo wake katika madai ya uongo. Vizuri.” Huo ndio ujumbe Trump aliandika kwa kejeli Alhamisi asubuhi katika akaunti yake ya Twitter.

Katika ujumbe wa pili wa tweet, Trump alisema, “ Mnashuhudia moja katika juhudi kubwa za kumtafuta mchawi katika historia za siasa za Marekani- ikiongozwa na baadhi ya watu wabaya na wenye utata.!”

Aidha Mueller pia anachunguza mahusiano ya mkwe wa Rais ambaye pia ni mshauri wake wa juu, kuhusiana na fedha na biashara zake.

Gazeti la Washington Post limeripoti Alhamisi kuwa uchunguzi dhidi ya Kushner katika malipo ya kifedha aliokuwa amefanya.

Habari zilizochapishwa awali zilitaja mikutano ya Kushner na viongozi wa bank ya maendeleo inayomilikiwa na Russia. Mawakili wa Kushner wanasema atashirikiana katika uchunguzi huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG