Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 15:11

Wachunguzi wa kesi ya Zuma waeleza alivyokuwa mdhaifu kwa Gupta


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Wachunguzi wa tuhuma za rushwa zinazomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wamesema kiongozi huyo wa zamani angefanya chochote ambacho familia ya Gupta mzaliwa wa India walitaka afanye kuanzia mwanzoni mwa muhula wake wa kwanza.

Tume inayofanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoenea wakati wa utawala wa miaka nane ya Zuma huko Afrika Kusini inayojulikana kama “ state Capture”, wamesema rais huyo wa zamani aliweka maslahi ya washirika wake mafisadi mbele kabla ya nchi yake.

Zaidi ya hapo imesema, Gupta alimtambua Zuma kama mtu mwenye tabia inayoweza kutumika kinyume na Waafrika Kusini kwa ajili ya maslahi yao ya kibiashara.

Maelezo haya yalitolewa katika sehemu ya nne ya taarifa ya tume hiyo iliyotolewa Ijumaa imeonyesha jinsi Zuma alivyoajiri na kuwafuta kazi mawaziri muhimu katika uendeshaji wa uchumi wa nchi hiyo kwa amri ya familia ya Ghupta.

Zuma aliyekuwa Rais mwaka 2009 na familia ya Gupta iliyoingia kuishi Afrika Kusini mwaka 1993 wakati utawala wa wazungu wachache ulipokuwa ukiisha amekanusha kufanya makosa yoyote.

XS
SM
MD
LG