Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:22

Zuma amuunga mkono Putin katika mzozo wa Ukraine


Rais wa zamani Jacob Zuma (Picha na AP)
Rais wa zamani Jacob Zuma (Picha na AP)

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemuunga mkono Rais wa Russia Vladmir Putin katika mzozo wa Ukraine unaonendelea huko Ukraine akimuelezea kuwa ni mtu wa amani.

Mataifa ya Magharibi yameweka vikwazo dhidi ya Russia ikiwa ni pamoja na kufungia mali zake zilizoko katika mataifa ya kigeni kutokana na uvamizi wake kwa Ukraine.

Lakini Zuma alisema uamuzi wa Putin unastahili kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakfu wake.

“ Wote tunahitaji amani katika dunia hii, kwa hiyo tungependa kutoa ushauri kwa wale wanaohusika na kuleta amani haraka iwezekanavyo ili maisha yaokolewe, taarifa imesema.

Zuma alilazimishwa kuondoka madarakani na chama chake cha ANC-mwaka 2018, kufuatia tuhuma za rushwa, hata hivyo amekanusha kufanya kosa lolote.

XS
SM
MD
LG