Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:34

Wachambuzi waeleza changamoto za uchaguzi mpya Kenya


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Uamuzi wa Mahakama ya Juu Kenya kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais yaliotangazwa mwezi Agosti umepongezwa Ijumaa na wachambuzi wakiuita wa “kihistoria” na “mfano kwa dunia nzima.”

Lakini, wameonya kuwa katika siku 60 ambazo uchaguzi mpya lazima ufanyika utaleta changamoto nyingi ikiwemo shinikizo na wasiwasi katika jamii, hivyo basi viongozi lazima watumie busara na uadilifu unahitajika katika uchaguzi huo mpya.

Siku ya Ijumaa Mahakama ya Juu ilitoa uamuzi wa kushtusha kwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 kwa dosari mbalimbali.

Jaji Mkuu David Maraga amesema uamuzi wa wengi katika jopo la majaji sita, wakiwemo wawili waliopinga uamuzi huo, umegundua kuwa Rais Uhuru Kenyatta “alikuwa hajachaguliwa kihalali”, ukipelekea uchaguzi huo kuwa batili.

Kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga na Umoja wa upinzani wa NASA walifungua kesi mahakamani, wakidai kuwa mfumo wa kupeperusha matokeo ya kura ulikuwa umedukuliwa, na kuwa fomu kutoka katika vituo vya kupiga kura ambazo zilitakiwa kuthibitisha matokeo ya kieletroniki hazikuwekwa katika mfumo wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

“Huu ni uamuzi wa kihistoria, ni wa kwanza wa aina yake Afrika,” Murithi Mutiga, mchambuzi mkongwe mwenye makazi yake Nairobi katika shirika la International Crisis Group, amesema.

Mutiga amesema uamuzi huo “ unamaanisha kuwa Wakenya, jamii iliyo na uwazi zaidi katika Afrika, inapevuka polepole kufikia demokrasia ya kweli”.

Leo hivi upinzani unaweza kwenda mahakamani na kutegemea kupata haki yao,” ameongeza.

Kwa mujibu wa Nic Cheeseman, Profesa wa siasa za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Birmingham, waangalizi wengi walitegemea uamuzi wa kiconservative- sawa na ule uliofanyika mwaka 2013 ambapo Odinga alipeleka malalamiko yake mahakamani lakini akashindwa kesi.

XS
SM
MD
LG