Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 19:58

Waasi Syria wachukua udhibiti wa mji wa Aleppo


Waasi wakiingia katika kijiji cha Anjara magharibi mwa mji wa Aleppo huko Syria Novenba 28, 2024. Picha na AP
Waasi wakiingia katika kijiji cha Anjara magharibi mwa mji wa Aleppo huko Syria Novenba 28, 2024. Picha na AP

Waasi wa Syria wamevamia mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria wa Aleppo, baada ya kulipua mabomu mawili ya kwenye gari wakipamba ba majeshi ya serikali siku ya Ijumaa, kulingana na mfuatiliaji wa vita vya Syria na wapiganaji.

Waasi walikuwa wakielekea katika mji wa Aleppo kwa siku kadhaa, wamekamata miji na vijiji kadhaa wakiwa njiani.

Syrian Observatory for Human Rights, ambayo inafuatilia vita, wamesema waasi wamelipua mabomu mawili ya kwenye gari katika ukingo wa magharibi wa mji huo siku ya Ijumaa.

Kamanda wa waasi ametoa ujumbe uliorekodiwa katika mitandao ya kijamii akiwataka wakazi wa mji huo kushirikiana na vikosi vinavyosonga mbele

Forum

XS
SM
MD
LG