Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 05:33

Senegal yasitisha tena huduma za internet


Waandamanaji wakati wakipambana na polisi huko Dakar Febuari 9, 2024. Picha na GUY PETERSON / AFP
Waandamanaji wakati wakipambana na polisi huko Dakar Febuari 9, 2024. Picha na GUY PETERSON / AFP

Huduma za internet zimesitishwa Jumanne nchini Senegal kwa mara nyingine tena mwezi huu, wizara ya mawasiliano imesema, baada ya mamlaka ya usalama kuzuiya maandamanano yanayopinga kucheleweshwa uchaguzi wa rais mwezi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Februari.

Uamuzi wa Rais Macky Sally kusukuma mbele upigaji kura hadi mwezi Desemba umeitumbukiza Senegal katika mzozo ambao umesababisha vifo vya watu watatu kufuatia ghasia baina ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Hata hivyo Marekani na Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali kurejesha ratiba ya uchaguzi iliyokuwepo awali.

Maandamano mabaya yanayowakabili vijana dhidi ya maafisa wa usalama yameharibu sifa ya Senegal ambayo ilikuwa mfano wa utulivu katika Afrika Magharibi.

Waandishi habari walikusanyika nje ya makao makuu ya baraza la vyombo vya habari jana usiku na kueleza usikitifu wao kutokana na kuporomoka kwa misingi ya demokrasia nchini mwao Migui Marame Ndiaye, ni rais wa jumuiya ya waandishi wa habari vijana anaeleza.

“Maafisa wa usalama mara nyingi wanalenga wafanyakazi wa vyombo vya habari katika kazi zao, ingawa kazi zetu zinakubalika kikatiba, na za kwao pia zimekubalika pia na katiba ya Senegal kwa hiyo lazima tuone ni jinsi gani tunaweza kushirikiana.”

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa siku ya Jumanne amesema Senegal lazima ifanye uchaguzi mpya wa rais “karaka iwezekanavyo” na itumie nguvu zinazokubalika kupambana na waandamanaji.

“Ufaransa inatoa rambirambi kwa wale wenye ndugu zao waliopoteza maisha wakati wa maandamanao huko Senegal katika asiku za hizi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG