Hayo yamejiri wakati chama kikuu cha wafanyakazi kikianza mgomo mkubwa wa saa 24 kuihimiza serikali kufikia makubaliano na waandamanaji, ambao awali walikuwa wakijaribu kuzuia mkutano wa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu na vyombo vya Habari, wakichoma moto mbao huku wakibeba mabango na kucheza ngoma.
Safari za ndege, huduma za usafiri na hospitali zimetatizwa kwa kiasi kikubwa wakati waandamanaji wakimtaka waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuwarudisha nyumbani mateka 101 waliobaki kutoka Gaza, jambo linalodhihirisha mgawanyiko mkubwa ndani ya Israel kuhusiana na mbinu yake.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema siku ya Jumatatu kuwa hadhani Netanyahu inafanya juhudi za kutosha kufikia makubaliano. Biden amesema yuko karibu kuwasilisha ombi lake la makubaliano ya kuwarudisha mateka nyumbani.
Netanyahu anakabiliana na miezi ya maandamano na shinikizo kutoka kwa waziri wake wa ulinzi pamoja na majenerali wakuu na maafisa wa usalama.
Lakini amesistiza kuyabakisha majeshi ya Israel katika maeneo muhimu ya Ukanda wa Gaza baada ya vita kusitishwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy ametangaza ukusimamishwa kwa vibali 30 kati ya 350 vya Uingereza vya upelekaji wa silaha kwenda Israel siku ya Jumatatu, akisema hatua hiyo siyo vikwazo vya silaha.
Mamia ya waombolezaji walijipanga katika mitaa ya Jerusalem siku ya Jumatatu wakati wazazi wa mateka Mmarekani mwenye asili ya Israel aliyeuawa Hersh Goldberg-Polin wakipita katika msafara ya mazishi yake.
Goldberg-Polin alikuwa miongoni mwa watu 40 walichukuliwa mateka wakati wa shambulizi la Hamas lililolenga tamasha la Oktoba 7.
Mwili wake ulikuwa ni miongoni ile ya Waisraeli sita waliopatikana na majeshi ya Israel mwishoni mwa wiki, na kuzua wimbi la huzuni na ghadhabu na mgomo wa kitaifa ambao umesimamisha shughuli katika sehemu kubwa ya Israel.
Forum