Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 19:12

Netanyahu aapa kuzidisha mapambano dhidi ya Hamas


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Jumapili ameapa kuzidisha mapambano na Hamas baada ya jeshi la Israel kuopoa miili ya mateka sita, ambao wote inaonekana waliuawa kwa kupigwa risasi na wanamgambo hao wakati wanajeshi walipokuwa wakijaribu kuingia kwenye eneo lao huko Gaza.

“Wale wanaoua mateka hawataki makubaliano” ya kusitisha mapigano Gaza, Netanyahu amesema katika taarifa yake, akiwaambia viongozi wa Hamas kwamba “tutawawinda, tutawakamata na tutawamaliza.”

Msemaji wa jeshi, kamanda Daniel Hagari, amewaambia waandishi wa habari katika kikao kifupi, “kwa mujibu wa makadirio yetu ya awali, waliuwawa kikatili na magaidi wa Hamas muda mfupi kabla hatujawafikia.”

Walipatikana kwenye handaki katika mji wa kusini wa Rafah.

Kufikia jioni, Waisraeli wenye huzuni na hasira waliingia barabarani, wakiimba “Sasa! Sasa!” na kumtaka Netanyahu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas ili kuwarudisha mateka waliosalia nyumbani.

Forum

XS
SM
MD
LG