Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:37

Waandamanaji 75,000 wakusanyika New York kupinga mabadiliko ya hali ya hewa


Waandamanaji mjini New York

Darzeni za maelfu ya watu katika jiji la New York hapa Marekani, wameanza maandamano ya wiki moja ya kutaka kukomeshwa kwa matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia, zinazolaumiwa kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Maandamano hayo ya Jumapili yaliyopwewa jina la “March to End Fossil Fuels,” yaani matembezi ya kumaliza matumizi ya mafuta ghafi, yalihudhuriwa na wanasiasa kama vile mbunge wa Marekani Alexandria Ocasio-Cortez na waigizaji wa filamu, Ethan Hawke, Edward Norton na Kevin Bacon,kti ya wengine.

Ni utetezi uliolenga ufunguzi wa hafla ya 'Wiki ya Hali ya Hewa ya New York,' ambapo viongozi wa dunia katika biashara, siasa na sanaa wanakusanyika kabla ya mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa Jumatano wiki hii.

Waandamanaji walisema juhudi zao zilikuwa zikilenga zaidi viongozi wengi wa mataifa ambayo yanasababisha uchafuzi mkubwa zaidi wa mazingira kwa kuzalisha gesi ya kaboni.

Ilikadiriwa kwamba takriban watu 75,000 walishiriki maandamano ya Jumapili.

Hayo yanajiri wiki mbili baada ya mkutano mkuu wa hali ya hewa barani Afrika uliofanyika mjini Nairobi, Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG