Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 23:59

Vita vya Israel- Hamas: Juhudi za Upatanishi zaonyesha mafanikio


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) alipokutana na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani huko Lusail, Oktoba 13, 2023. Picha na REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) alipokutana na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani huko Lusail, Oktoba 13, 2023. Picha na REUTERS

Wapatanishi wa kimataifa wameonekana kupata maendeleo siku ya Jumatano katika kurefusha makubaliano huko Gaza.

Pamoja na kuwashawishi watawala wa Hamas wa eneo hilo kuendelea kuwaachilia mateka ili wafungwa wa Palestina waachiliwe

na kuuongeza muda kusita kwa mashambulizi ya anga na ardhini ya Israeli. Vinginevyo muda wake ungekwisha ndani ya siku moja.

Israel imekaribisha kuachiliwa kwa darzeni ya mateka katika siku za hivi karibuni na inasema itadumisha mapatano hayo ikiwa Hamas itaendelea kuwaachilia mateka.

Lakini lengo lake lingine kubwa – kuianamiza kundi lenye silaha ambalo limetawala Gaza kwa miaka 16 na kupanga shambulio la mauaji dhidi ya Israeli ambalo limekuwa chanzo cha vita - inaonekana uwezekanowa kuendelea ni mdogo.

Wiki kadhaa za mashambulizi ya anga na uvamizi wa ardhini yameharibu maeneo mengi yaliyoko kaskazini mwa Gaza na kuua maelfu ya Wapalestina.

Lakini inaonekana kuwa na athari ndogo kwa utawala wa Hamas, ikithibitishwa na uwezo wake wa kufanya mazungumzo magumu, kutekeleza usitishaji mapigano kati ya makundi mengine yenye silaha, na kupanga kuachiliwa huru kwa mateka.

Uvamizi wa ardhini wa Israel upande wa kusini huenda hatimaye ukawafukuza viongozi wa Hamas na kuvunja miundo mbinu iliyosalia ya wanamgambo hao, ikiwa pamoja na kilomita za mahandaki, lakini kwa gharama ya maisha ya Wapalestina na uharibifu ambao Marekani, mshirika mkuu wa Israel anaonekana hayuko tayari kuushuhudia.

Forum

XS
SM
MD
LG