Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:29

Wanamgambo wa Hamas wamewaachia huru mateka zaidi walioshikiliwa Gaza


Wanamgambo wa Hamas wamewaachia mateka zaidi huko Gaza
Wanamgambo wa Hamas wamewaachia mateka zaidi huko Gaza

Jeshi la Israel limesema mateka 12 waliokuwa wakishikiliwa Gaza, Waisraeli 10 na raia wawili wa kigeni walipelekwa Israel.

Wanamgambo wa Hamas wamewaachia huru mateka zaidi wa Israel katika siku ya tano ya makubaliano yaliyoongezwa hadi siku sita ili kusitisha mapigano kati ya Israel na hamas Muda mfupi baadaye, taifa la Kiyahudi liliwaachia huru wafungwa zaidi wa Kipalestina.

Jeshi la Israel limesema mateka 12 waliokuwa wakishikiliwa Gaza, Waisraeli 10 na raia wawili wa kigeni walipelekwa Israel. Israel iliwaachia huru wafungwa 30 wa Kipalestina, wanawake 15 na vijana 15 kutoka gereza la Ukingo wa Magharibi na kituo cha mahabusu cha Jerusalem, kulingana na Palestinian Prisoners Club, ambalo ni shirika lisilo rasmi.

Forum

XS
SM
MD
LG