Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:12

Viongozi - NRM wagawanyika juu ya ukomo wa umri wa urais


Sakata la kubadilisha ukomo wa umri wa urais lililotokea hivi karibuni katika bunge la Uganda.
Sakata la kubadilisha ukomo wa umri wa urais lililotokea hivi karibuni katika bunge la Uganda.

Viongozi wa chama tawala cha NRM huko Buzaaya, Wilaya ya Kamuli wamepiga kura dhidi ya hatua iliyosubirishwa ya kuondoa ukomo wa umri kwa kinyang’anyiro cha urais kutoka katika Katiba ya Uganda.

Viongozi hao wamepitisha azimio wakati wa mkutano wao wa ushauri Jumamosi ulioitishwa na wabunge wa Buzaaya, Isaac Musumba katika ukumbi wa Taasisi ya Ufundi eneo la Nawanyago.

Mkutano huo wa mashauriano ulikusudia kuwahamasisha wakereketwa wa chama cha NRM wakubaliane na marekebisho ya ukomo wa urais ambayo yalisubirishwa.

Marekebisho hayo ya Katiba kwa Waganda wengi yalionekana kama ni mbinu ya kumpa mwanya Rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena nafasi ya urais 2021,

Hata hivyo mkutano huo uligeuka kuwa ni vurugu wakati viongozi wa chama hicho katika eneo hilo Buzaaya walipowazuia baadhi ya wanachama kuingia katika eneo hilo.

Wachambuzi wa kisiasa wanakubaliana kuwa iwapo Katiba haitofanyiwa marekebisho, Museveni hatoweza kuwa na sifa za kugombea kwani ukomo wa umri wa wagombea urais hivi sasa ni miaka 75.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimesema kuwa watu waliozuiwa kuingia katika mkutano huo walitishia kukihama chama cha NRM na kwenda upande wa upinzani kwa sababu NRM ilikuwa imeamua kuwafanya wawe “mayatima”.

“Rais Museveni alikwenda msituni kupigana dhidi ya madikteta ambao walikuwa wananang’ania kubakia madarakani na aliahidi kuirudisha demokrasia nchini. Rais Museveni hivi leo anakubali utashi wake kumyumbisha dhidi ya mabadiliko ya msingi aliyokuwa ameyaanzisha yeye mwenyewe. Anatakiwa kuacha athari njema katika chama cha NRM," amesema Hamis Dheyongera, Diwani wa NRM eneo la Wankole.

XS
SM
MD
LG