Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:52

Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya Russia


Makamu wa Rais Mike Pence akipongezana na Waziri Mkuu wa Georgia Georgy Kvirikashvili
Makamu wa Rais Mike Pence akipongezana na Waziri Mkuu wa Georgia Georgy Kvirikashvili

Makamu Rais wa Marekani, Mike Pence amesema hatua za kidiplomasia zilizochukuliwa na Russia kujibu vikwazo vipya hazitaizuilia nia ya dhati ya Marekani kuimarisha usalama wake na ule wa washirika wake.

Akizungumza Jumanne katika ziara yake huko Georgia, Pence alisema mswada wa vikwazo hivyo ambapo hivi karibuni Rais Donald Trump atasaini karibuniunapeleka “ujumbe wa wazi” kwamba harakati za Russia nchini Ukraine na ushirikiano wake na Iran na Syria, ni lazima msimamo wake huo ubadilika.

Bunge kwa pamoja lilipitisha kwa idadi kubwa mswada wenye vikwazo vinavyoiadhibu Russia kwa kuingilia kati uchaguzi wa Marekani mwaka 2016, huku pia ikiweka vikwazo vipya kwa Iran na Korea Kaskazini.

Russia ilijibu vikwazo hivi kwa kuiamuru Marekani kupunguza idadi ya wafanyakazi wake zaidi ya 1,200 waliopo Russia hadi kufikia watu 755.

“Rais na Bunge letu wako pamoja katika ujumbe wetu kwa Russia: mahusiano bora na kuondolewa kwa vikwazo, kutaitaka Russia kubadilisha maamuzi yake ambayo yamepelekea kuwekewa vikwazo tangia awali,” amesema Pence.

Pence katika ziara yake kwa mataifa kadhaa inakusudio la kuonyesha ushirikiano wa Marekani na washirika wake katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG