Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 02:49

Vijana 1000 wa Afrika washiriki kwenye programu ya Obama


Winnie Singwa
Winnie Singwa

Vijana wapatao 1000 walishiriki katika mafunzo ya wiki sita nchini Marekani katika vyuo mbali mbali ikiwa ni mpango ulioanzishwa na rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ujulikanao kama Mandela Washington Fellow.

Baada ya kukamilisha masomo yao vijana hawa walikutanishwa katika mkutano wa siku 4 uliofanyika katika hoteli ya Marriot Marquiz mjini Washington Dc.

Mkutano huo ulikamilika Alhamisi Agosti 3, 2017 na baadhi ya vijana hao kuanza safari ya kurudi nyumbani na wengine wakiendelea kubaki Marekani kwa mwendelezo wa masomo ya uzoefu kwenye vituo mbali mbali vya kazi.

Baadhi ya washiriki wa programu ya Obama
Baadhi ya washiriki wa programu ya Obama

Vijana hawa wametoka katika nchi 49 barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na wamepitia usaili wa hali ya juu kabla ya kupata fursa hii.

Akizungumza na vijana hao mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia na masuala ya Afrika Seneta Chris Coons wa Delaware amesema kwa jumla vijana waliopeleka maombi walikuwa wapatao 60,000 lakini waliopata fursa hii ni vijana 1000 tu.

Na akawapa moyo kwamba wao ndio viongozi wa kesho wa Afrika na itakuwa vizuri Wamarekani nao wapate uzoefu kama huo kwa kwenda kutembelea bara la Afrika.

Aidha seneta akijibu swali la mmoja wa vijana hao kuhusu ufanyaji kazi wa vyombo vya habari vya Marekani na mtazamo hasi kwa Afrika, alikubaliana na kijana huyo kwamba vyombo vya Marekani vinaripoti yale yalio mabaya tu ya Afrika na kuwataka vijana hao kuchukua fursa ya kutangaza mazuri yaliopo barani Afrika.

Vijana hao walipata nafasi sio tu kwa kazi za kujisaidia bali pia jamii iliyowazunguka , kwa hiyo vijana waliokuja hapa ni pamoja na madaktari bingwa, wauguzi, wajasiriamali, marubani, wanasheria, watalaam wa teknohama , wahandisi, wanaharakati mbali mbali wa haki za kijamii, wanawake , watoto n.k.

Pia vijana hawa wameweza kujipatia mambo mengi ambayo watarudisha nyumbani Afrika, mmoja wao ni daktari bingwa wa kansa kutoka Tanzania Heri Tungaraza ambaye alipata nafasi kujifunza kutoka katika hospitali zinazoongoza katika matibabu ya kansa nchini Marekani huko katika chuo kikuu cha Emory Georgia na Cancers Centers of America waliko madaktari bingwa wa kansa.

Daktari huyu anasema amepata mbinu za madaktari wa Marekani ambao wanafanya kazi kwa kushauriana kama timu , akisema“si mpaka mmoja ashindwe ndio atafute mwenzie wasaidiane mawazo” anasisitiza kwambaatalipeleka hilo kwenye kliniki na hospitali za nchi yake Tanzania ili madaktari wafanye kazi kama timu kwani kuunganisha kichwa zaidi ya kimoja ni kitu kizuri na madaktari wapeane mawazo aliongeza.

Vijana hawa wameweza kufanikiwa pia kushirikiana uzoefu wa yale mambo mbali mbali wanayofanya katika nchi zao na pia hadithi za maisha yao kwa mfano Winnie Singwakutoka Kenya anasema alikua akiwa yatima baada ya kupoteza wazazi wake akiwa na umri wa miaka 6 tuna alipelekwa kulelewa na shangazi yakeambaye alimtesa sana kumfanyisha kazi za ndani kupita kiasi , kumtenga n.k, akashindwakwenda kwa shangazi mwingineambaye kwa bahati mbayaalifiwa na mume wake. Kwa hiyo akajikuta anaangukia mitaani akiwa na umri wa miaka 8 tu na anasema alilala kila mahali na alisumbuliwa sana na wanaume, makondata wa matatu, waendesha piki piki , wasio na ajira n.k huku akajikuta anaanza kutumbukia kwenye kuvuta sigara na mambo mengine.

Lakini kijana huyu maisha yake yalikuja kubadilika baada ya kuchukuliwa na shirika la Compassion International ambao walimchukua akiwa na umri wa miaka 10 na kumrudisha shulenina kumpa malezi hatimaye alisoma shule ya msingi, sekondari mpaka chuo kikuu na kuchukua masomo ya Sosholojia.

Sasa ameamua kurudi na kusaida jamii yake akisaidia wasichana wapatao 500 katika kituo chao ambao ni yatima wakiwapa nafasi ya kusoma shule na kuwafundisha kuwa watoto wenye tabia njema wakisaidia hata wale waliopata uja uzito wakiwa wadogo na kufukuzwa makwaobaada ya kupitia yote hayo sasa anatoa mchango wake kwa jamii yake.

XS
SM
MD
LG