Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Utawala wa sheria, uhuru wa habari mashakani Tanzania?


Maalim Seif Shariff Hamad
Maalim Seif Shariff Hamad

Wabunge wa chama cha upinzani CUF wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Habari nchini Tanzania kujitokeza na kutoa tamko juu ya shambulizi lililofanyika Jumamosi katika mkutano wa Chama cha Upinzani.

Mbunge huyo ametaka Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na Waziri wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kutoa maelezo juu vitendo hivi vya uvunjifu wa amani vilivyojitokeza na hatua zinazochukuliwa kukomesha matukio haya. Shambulizi hilo liliwalenga wanasiasa na waandishi wahabari walikuwepo kwenye mkutano huo.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao Jumapili, naibu mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, Ali Salehe amesema haisawiriki tukio la uvunjifu wa amani likatokea katika nchi inayothamini utawala wa sheria na uhuru wa kujielezea.

Kambi ya upinzani pia imelaani shambulizi la mkutano wa viongozi wa CUF upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif na waandishi wa habari na kutaka serikali ichukue hatua kukomesha matukio haya ya uvunjifu wa amani.

Katika mkutano huo Salehe alikuwa na wabunge wenzake wanne na amesema chama hicho kimeshtushwa na kuvamiwa kwa mkutano na watu waliokuwa na silaha na bastola akieleza kuwa tayari jambo kama hilo limetokea kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye.

XS
SM
MD
LG