Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:47

Korea Kaskazini yamshikilia raia mwengine wa Marekani


Bendera ya Korea Kaskazini yapepea katika ubalozi wake Jijini Beijing
Bendera ya Korea Kaskazini yapepea katika ubalozi wake Jijini Beijing

Raia mwengine wa Marekani amekamatwa nchini Korea Kaskazini.

Mtu huyo Mkorea-Mmarekani amekamatwa Ijumaa huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Pyongyang alipokuwa anajitayarisha kuondoka nchini, shirika la habari la Yonhap limeripoti Jumapili.

Akiwa ameweza kutambulika kwa jina moja la ubini wake kama Kim, mtu huyo amerepotiwa kuwa alikuwa akizungumzia masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Korea Kaskazini kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Hata hivyo sababu za kushikiliwa kwake hazikuweza kujulikana mara moja.

Kushikiliwa kwake kunafanya idadi ya Wamarekani wanaoshikiliwa Korea Kaskazini kufikia watu watatu.

Korea Kaskazini siku za nyuma iliwashikilia raia wa Marekani ikiwatumia kama ni turufu ya mazungumzo yake na Marekani.

Wamarekani wengine wawili bado wanashikiliwa Korea Kaskazini. Mwaka jana, Otto Warmbier, wakati huo akiwa na miaka 21 mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Virginia katika mji mdogo wa Cincinnati, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu baada ya kukiri kutaka kuiba bango la propaganda.

Kwa upande wake Dong Chul, ambaye alizaliwa Korea Kusini lakini anasaidikiwa kuwa na uraia wa Marekani, anatumikia kifungo cha miaka kumi kwa tuhuma za ujasusi.

Angalau raia mmoja mwengine wa kigeni, mchungaji wa Canada, pia anazuiliwa na Korea Kaskazini.

Hyeon Soo Lim, ambaye ni mzaliwa wa Korea Kusini na raia wa Canada mwenye umri wa miaka 60, alikutikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2015 kwa tuhuma za kujaribu kutumia dini kuangamiza mfumo wa nchi ya Korea Kaskazini na kuzisaidia serikali za Marekani na Korea Kusini kuwarubuni na kuwateka raia wa Korea Kaskazini.

XS
SM
MD
LG