Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:47

Uvujaji Siri Waikumba Serikali ya Trump, Je Utaendelea?


Rais Donald Trump akijibu maswali ya waandishi White House, Washington, Feb. 16, 2017.
Rais Donald Trump akijibu maswali ya waandishi White House, Washington, Feb. 16, 2017.

Uongozi wa Rais Donald Trump umekasirishwa na uvujaji wa habari za siri ulioanza kabla ya Trump kuapishwa kuwa rais.

Lakini namna ya utoaji siri hizo zisizoruhusiwa unaokiuka taratibu ni tofauti kwa namna fulani katika utawala huu ukilinganisha na kuvuja kwa habari zilizowaudhi au kuwakasirisha marais wengine wa Marekani.

Uvujaji wa taarifa hizi mapema, ikiwemo sera za siri, au amri za kiutendaji au mipango – sio kitu kigeni, kwa mujibu wa Louis Clark, mkurugenzi mtendaji wa mradi wa serikali wa uwajibikaji, taasisi isiyo ya kibiashara iliyojitolea kuwatetea watoa taarifa.

Clark ameiambia VOA kuwa kitu kipya ni kusudio la wanaovujisha siri—wale wanaotoa habari, mara nyingi kwa waandishi wa habari.

Clark amesema mara nyingi uvujishaji siri unafanywa na uongozi kwa kusudio la “ kuweka shinikizo kwa maamuzi fulani ya kisiasa au ya kisera.”

Kitu ambacho ni tofauti katika suala hili wakati huu wa uongozi wa Trump, ameongeza, ni ile hisia iliyoko kwa watu wengi kwamba uvujaji wa siri unakusudia kumchafua rais na heshima yake.

Kukosolewa rais moja kwa moja katika mwenendo huu “ haujawahi kutokea,” Clark ameiambia VOA.

Watoa Taarifa

Jesselyn Radack ni wakili mstaafu wa Wizara ya Sheria Marekani aliyejikita katika masuala ya usalama wa taifa na haki za binadamu ambaye hivi sasa anafanya kazi kwenye programu ya kuwalinda watoa taarifa na vyanzo vya habari, ilioundwa na taasisi ya utoaji sahihi wa taarifa za umma.

Yeye anapinga kuwa kuna “hatari zaidi” kuhusu kuvuja siri za Trump kuliko yale yaliyokusudiwa dhidi ya Rais mstaafu Barack Obama, ambaye uongozi wake ulikumbwa na uvujaji wa siri nyingi za kitaifa katika historia ya Marekani.

“Aghlabu, majaribio ya uvujashaji siri za uongozi unaongeza kasi msukumo wa fikra za kisera,” Radack ameiambia VOA katika mahojiano.

“Uvujaji wa siri za Trump zinaonekana kuwa hatari zaidi. Ziko kila sehemu, Hazionyeshi kuwa ni za Kimkakati.”

Shinikizo la Kujiuzulu Flynn

Habari zilizovuja zilisababisha matatizo kwa mtu wa kwanza wiki hii ambapo mshauri wa usalama wa taifa wa Trump, Jenerali Michael Flynn alishinikizwa kujiuzulu.

Katika mlolongo wa tweets Jumatano asubuhi, Trump amesema uvujishaji wa siri ndio uliosababisha Flynn kuondoka madarakani akifananisha uvujaji huo na mbinu zinazotumiwa Russia. Pia ameshutumu “vyombo vya habari feki” Kwa kuendelea kutumia taarifa za siri kukuza “nadharia zao za uzushi na chuki potofu.”

Fedheha kubwa hapa ni habari za siri zinatolewa kinyume cha sheria na “idara za ujasusi” kama peremende. Hilo ni kukosa uzalendo kabisa” Trump ameandika.

XS
SM
MD
LG