Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:11

Uvamizi wa Russia: Rais wa Ukraine awatembelea wanajeshi walioko mstari wa mbele


Rais Zelenskyy awapongeza wanajeshi wa Ukraine walioko mstari wa mbele vitani.
Rais Zelenskyy awapongeza wanajeshi wa Ukraine walioko mstari wa mbele vitani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumanne amewatembelea wanajeshi walioko mstari wa mbele.

Bila ya kuelezea eneo walipo, Zelenskyy alibandika katika Telegram picha kadhaa akiwa na wanajeshi.

“Walinzi wetu. Mstari wa mbele. Leo niko hapa kuwapongeza wapiganaji wetu katika Siku ya Wanajeshi wa Majini wa Ukraine,” Zelenskyy alisema.

“Akirejea kutoka katika ziara yake ya nje ya nchi, Rais Volodymyr Zelenskyy alitembelea maeneo mbalimbali ya mstari wa mbele ambako majeshi ya Ukraine yanailinda nchi katika eneo la Vugledar-Maryinka katika mkoa wa Donetsk,” Taarifa ya ofisi ya rais ilisema.

Kiongozi huyo wa Ukraine amefanya ziara kadhaa katika maeneo ya mstari wa mbele tangu Russia ilipofanya uvamizi kamili mwaka 2022.

Katika wiki za hivi karibuni, ziara zake zimekuwa katika miji mikuu ya Ulaya kupata ahadi mpya za misaada ya kijeshi na kuwaeleza washirika umuhimu wa kupeleka ndege za kisasa Zaidi za kivita kuyasaidia majeshi ya Ukraine.

Waziri wa Jeshi la Anga Marekani Frank Kendall alisema “ itachukua miezi kadhaa” kuamua kupeleka ndege aina ya F-16 huko Ukraine.

Ripoti hii imechangiwa na mwandishi wa Masuala ya Usalama wa Taifa Jeff Seldin. Na baadhi ya taarifa za ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari vya AP, AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG