Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:29

Kellogg Akaimu Nafasi ya Mshauri wa Usalama wa Taifa Marekani


Mstaafu Luteni Jenerali Keith Kellogg
Mstaafu Luteni Jenerali Keith Kellogg

Rais Donald Trump amemteua mstaafu Luteni Jenerali Keith Kellogg kuwa kaimu mshauri wa usalama wa taifa baada ya Jenerali mstaafu Michael Flynn kujiuzulu Jumatano usiku.

Kabla ya hapo Kellogg alikuwa ameteuliwa mkuu wa wafanyakazi katika Baraza la Usalama la Taifa na alikuwa mshauri wa Trump wakati wa kampeni za uchaguzi.

Duru za habari zinasema kuwa Trump pia anafikiria kuwapa nafasi hiyo kati ya aliyekuwa mkurugenzi wa CIA David Petraeus au Naibu Admirali wa majeshi ya majini, Robert Howard kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa uongozi wa Trump.
Maelezo ya Timu ya uongozi ya Trump kuhusu mazungumzo ya Flynn na Balozi wa Russia yalikuwa yakibadilika badilika katika wiki kadhaa, likiwemo suala la mara ngapi waliwasiliana, tarehe za mawasiliano hayo na kile kilicho ongelewa.

White House Ilitahadharishwa

Mwisho wa mwezi uliopita, Idara ya Sheria iliitahadharisha White House kuwa Flynn inawezekana atakuwa amedhibitiwa na Russia.

Tahadhari hiyo ilionyesha kuwepo mgongano kati ya kile kilichokuwa kinafahamika na umma kuhusu mazungumzo ya simu na kile maafisa wa kijasusi walichokuwa wakikijua kutokana na mazungumzo yaliyokuwa yamerekodiwa kati ya Flynn na balozi wa Russia.

Mazungumzo hayo yalirekodiwa na maafisa hao kama ni sehemu ya ufuatiliaji wa kawaida unaofanywa na chombo cha ujasusi kwa maafisa wa kigeni katika mazungumzo yao yote wakiwa nchini Marekani.

Afisa wa Marekani ameliambia Shirika la Habari la Associated Press kwamba Flynn alikuwa katika mawasiliano mara nyingi na balozi Sergey Kislyak ikiwemo siku ambayo uongozi wa Obama ulipo iwekea vikwazo Russia kwa kuvuruga uchaguzi, na vile vile wakati mwengine ni serikali hiyo ilipokuwa kwenye mpito kukabidhi madaraka.

Afisa wa uongozi uliopo madarakani na watu wengine wawili ambao walikuwa wanajua hali hii wamethibisha hilo, kwa sharti la kutotajwa kwani hawaruhusiwi kulizungumzia hadharani.

Wamesema walikuwa wanafahamu tahadhari iliotoka Idara ya Sheria. Hata hivyo haikufahamika lini Trump na Pence walijua suala hili la Idara ya Sheria lililofikishwa kwao.

Kashfa ya Flynn

Jenerali mstaafu Michael Flynn, alijiuzulu kufuatia kashfa iliyomkumba kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na balozi wa Russia nchini Marekani, Sergey Kislyak, ambayo yalikuwa yamezua utata na mjadala mkubwa Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Flynn, aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Donald Trump Jumatatu usiku.

Katika barua yake Flynn amesema alifanya mawasiliano kadhaa na balozi wa Russia wakati wa kipindi cha mpito, na kumpa Makamu wa Rais, Mike Pence "habari ambazo hazikukamilika."

Makamu wa Rais

Makamu wa Rais ambaye alitegemea habari alizopata kutoka kwa Flynn awali alisema mshauri wa usalama wa taifa hajafanya majadiliano kuhusu vikwazo na balozi wa Russia, ingawaje baadaye Flynn alikiri kuwa suala hilo huenda lilijitokeza katika mazungumzo yao.

Tuhuma zilikuwa zimeibuka kuwa Flynn, ambaye alikuwa amehudumu kwenye wadhifa huo kwa takriban mwezi mmoja, alizungumza na balozi huyo mnamo mwezi Desemba, kuhusu vikwazo ambavyo Marekani iliiwekea Russia, licha ya kuwa rais Barack Obama bado alikuwa mamlakani na kwamba Trump hakuwa ameapishwa kama rais.

XS
SM
MD
LG