Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:44

Mshauri wa Usalama wa Taifa Marekani Michael Flynn ajiuzulu


Mshauri mkuu wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jenerali Michael Flynn, aliyejiuzulu mnamo tarehe 13, Februari, 2017.
Mshauri mkuu wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jenerali Michael Flynn, aliyejiuzulu mnamo tarehe 13, Februari, 2017.

Mshauri wa Usalama wa taifa Marekani, Jenerali mstaafu Michael Flynn, amejiuzulu Jumatatu usiku kufuatia kashfa iliyomkumba kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na balozi wa Russia nchini Marekani, Sergey Kislyak, ambayo yalikuwa yamezua utata na mjadala mkubwa Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Flynn, aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Donald Trump Jumatatu usiku.

Katika barua yake Flynn amesema alifanya mawasiliano kadhaa na balozi wa Russia wakati wa kipindi cha mpito, na kumpa Makamu wa Rais, Mike Pence "habari ambazo hazikukamilika."

Makamu wa Rais ambaye alitegemea habari alizopata kutoka kwa Flynn awali alisema mshauri wa usalama wa taifa hajafanya majadiliano kuhusu vikwazo na balozi wa Russia, ingawaje baadaye Flynn alikiri kuwa suala hilo huenda lilijitokeza katika mazungumzo yao.

Tuhuma zilikuwa zimeibuka kuwa Flynn, ambaye alikuwa amehudumu kwenye wadhifa huo kwa takriban mwezi mmoja, alizungumza na balozi huyo mnamo mwezi Desemba, kuhusu vikwazo ambavyo Marekani iliiwekea Russia, licha ya kuwa rais Barack Obama bado alikuwa mamlakani na kwamba Trump hakuwa ameapishwa kama rais.

XS
SM
MD
LG