Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 03:12

Utawala wa kijeshi Burkina Faso wawaweka kizuizini maafisa wanne


Waziri wa Nchi wa Burkina Faso Bassolma Bazie akihutubia mkutano wa 78 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Septemba 23, 2023. Picha na Leonardo Munoz / AFP.
Waziri wa Nchi wa Burkina Faso Bassolma Bazie akihutubia mkutano wa 78 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Septemba 23, 2023. Picha na Leonardo Munoz / AFP.

Burkina Faso ilisema siku ya Alhamisi kuwa maafisa wanne wametiwa ndani, siku moja baada ya serikali ya kijeshi kutangaza kuwa imezima jaribio la mapinduzi.

Watu hao wanne wanashukiwa kuhusika na "njama dhidi ya usalama wa serikali", mwendesha mashtaka wa kijeshi Ahmed Ferdinand Sountoura alisema katika taarifa ambayo shirika la habari la AFP imeiona siku ya Alhamisi.

Wengine wawili "wako mafichoni" kulingana na taarifa hiyo.

Utawala wa kijeshi ulisema Jumatano jioni kuwa idara za upelelezi na usalama zilizuia jaribio la mapinduzi.

Tukio hili limetokea takribani mwaka mmoja tangu kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traore anyakue mamlaka katika taifa hilo la Afrika Magharibi Septemba 30, 2022.

Kuchukua kwake madaraka ilikuwa ni katika mapinduzi ya pili ya nchi hiyo ndani ya kipindi cha miezi minane –kwa sehemu fulani yote yakichochewa na kutoridhika na kushindwa kukomesha uasi wa wanajihadi, ambao wameingia nchini humo wakitokea nchi jirani ya Mali mwaka 2015.

Mwendesha mashtaka wa kijeshi amemtaka mtu yeyote aliye na taarifa zinazoweza "kuchangia udhihirisho wa ukweli aje kutoa ushahidi".

Jumanne jioni, maelfu ya watu walikuwa wameingia katika mitaa ya mji mkuu Ouagadougou kufuatia mwito kutoka kwa wafuasi wa Traore "kumtetea" wakati kuna uvumi wa kutokea mapinduzi kwenye mitandao ya kijamii.

Traore aliingia kwenye mtandao wa X, uliokuwa ukijulikana kama Twitter, Jumatano na kusisitiza "azimio lake la kuongoza kipindi cha mpito kwa usalama mbali na matatizo na kutumia hila tofauti za kukomesha maandamano yetu yasiyoweza kuepukika ya kuelekea kujitawala".

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG