Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:26

Ushahidi zaidi juu ya Lissu watolewa kanisani Tanzania


Madai zaidi yalitolewa Jumapili kuhusu kufuatiliwa kwa gari la mbunge wa upinzani Tundu Lissu kabla ya kushambuliwa kwa risasi mjini Dodoma Septemba 7,

Madai hayo yalitolewa na mdogo wake mbunge huyo, Vincent, wakati anazungumza katika ibada ya kumwombea kaka yake katika kanisa la Ufufuo na Uzima mjini Dar es salaam

Amesema alimwona kaka yake akiwa amelala kitandani hospitalini mwili ukiwa na damu.

Vincent amesema alikwenda Dodoma kuwashukuru madaktari waliofanya kila waliloweza kuokoa maisha ya ndugu yake.

Amesema kaka yake ni mpenda haki tangu akiwa mdogo na ameomba wananchi wazidi kumuombea.

Lissu hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi nchini Kenya.

Katika shambulio lililofanywa na watu wasiofahamika nyumbani kwa Lissu Area D mjini Dodoma, mbunge huyo alipigwa risasi tano.

XS
SM
MD
LG