Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:42

Pence apongeza uhuru, ushiriki wa dini mbalimbali Indonesia


Makamu wa Rais Mike Pence
Makamu wa Rais Mike Pence

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence ameisifia Indonesia kwa kile alichokiita taifa lenye "utamaduni wa Uislamu wenye kuvumilia itikadi nyingine”.

Amesema hayo wakati akifanya ziara nchini humo Alhamisi ambapo anafanya mazungumzo na Rais Joko Widodo na maafisa wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-mashariki ya Asia.

“Ikiwa ni taifa la pili na kubwa zaidi katika democrasia duniani, nchi zetu mbili zinashirikiana katika maadili ya pamoja ikiwemo uhuru, utawala wa sheria, haki za binadamu na kuwepo kwa ushiriki wa dini mbalimbali.

Marekani inajivunia kuwa na ushirikiano na Indonesia, katika kuendeleza na kulinda maadili hayo,” amesema Pence.

Pia amesisitiza umuhimu wa “suala la msingi la uhuru wa utumiaji wa maeneo ya anga na bahari,” na kusema kuwa yeye na Rais Donald Trump wanataka kupanua mahusiano ya kibiashara na Indonesia.

“Chini ya uongozi wa Rais Trump Marekani inataka mahusiano ya kibiashara ambayo ni huru na haki. Hilo ni kwa ajili ya kutengeneza ajira na kukuza uchumi kwa pande zote.

“Kama vile wewe, Rais Widodo ulivyosema mara nyingi, tunatafuta mahusiano yatakayonufaisha pande zote mbili na tunaamini kuwa tunaweza kufikia hilo kwa kuendeleza mwanzo huu,” Pence amesema.

Ikiwa ni sehemu ya ziara yake, Pence pia ametembelea Msikiti wa Istiqlal ulioko Jakarta, ambao ni mkubwa kuliko misikiti yote ya Kusini-mashariki ya bara la Asia, na amekutana na viongozi wa dini kutoka madhehebu kadhaa, wakiwemo Waislamu, Wakristo, Mabuda na Wahindu.

Indonesia ni nchi yenye Waislamu wengi zaidi, na hii ni nchi ya tatu Pence kuzuru baada ya kutokea Korea Kusini na Japan. Pia anatarajiwa kuelekea Australia ikiwa ni sehemu ya ziara yake.

XS
SM
MD
LG