Hadi kufikia Jumatatu idadi rasmi ya watu waliokuwa ndani ya meli ya Spice Islander iliyozama kati ya Unguja na Pemba haikujulikana. Hata hivyo hivyo wengi kati ya zaidi watu 500 walionusuriuka wamekuwa wakizungumza na vyombo vya habari kueleza mkasa uliowafika.
Mmoja kati ya walionusurika Ameir Rashid ambaye amewapoteza wazazi wake pamoja na ndugu zake wanne, alizungumza na Sauti ya Amerika na kueleza matukio kabla na baada ya ajali.
Abiria mwingine aliyenusurika alikuwa Mzee Said Rashid anaeleza kile alichoshuhudia na kile alichofanya hadi kufika pwani.