Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:43

USAID kuipatia Kenya $255 kupambana na ukame


Mkuu wa shirka la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa, USAID, Samantha Power (Kushoto) na waziri wa wa huduma za umma, jinsia na wazee, Margaret Kobia.
Mkuu wa shirka la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa, USAID, Samantha Power (Kushoto) na waziri wa wa huduma za umma, jinsia na wazee, Margaret Kobia.

Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa USAID limetangaza kwamba litaipatia Kenya dola milioni 255 kama msaada wa dharura na maendeleo kukabiliana na ukame uliokithiri.

Akitangaza msaada huo, msimamizi mkuu wa USAID, Samantha Power, amewaambia wanahabari jijini Nairobi kwamba kiasi hicho kinajumuisha dola milioni 65 ambazo tayari USAID ilikuwa imetoa mwaka huu.

Serikali ya Kenya inasema watu milioni 4.1 katika taifa hilo la Afrika Mashariki Mashariki wanakabiliwa na uhaba wa chakula, ambalo ni ongezeko kutoka milioni watu 3.8 mwezi Machi mwaka huu.

Power alisema vita vya Ukraine vinaongeza mateso nchini Kenya na maeneo mengine.

Margaret Kobia, waziri wa Kenya anayehusika na huduma za umma, jinsia, masuala ya wazee na programu maalum, alisema hadi sasa serikali imetumia shilingi bilioni 12.6, sawa na dola za Marekani milioni 106.28, kusaidia watu walioathiriwa na ukame lakini kulikuwa na upungufu wa shilingi bilioni 15.

XS
SM
MD
LG