Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:57

WFP laitisha fedha zaidi ili kutoa chakula kwa Zimbabwe


Watu wa Zimbabwe wapokea chakula kutoka WFP
Watu wa Zimbabwe wapokea chakula kutoka WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema linahiataji takriban dola milioni 65 ili kupunguza ukosefu wa usalama wa chakula nchini Zimbabwe.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema tathmini yake imeonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 5 katika taifa hilo la kusini mwa Afrika wanatarajia kushuhudia uhaba wa chakula katika miezi ijayo.

Belinda Popovska, msemaji wa WFP, Zimbabwe, ameiambia VOA kwamba shirika hilo limeanza kuangalia kupata ufadhili kwa ajili ya kuagiza chakula kwa wale wanaohitaji.

Belinda anasema ripoti za karibuni za mwaka huu katika maeneo ya vijijini nchini Zimbabwe, iliyotolewa na kamati ya tathmini imeashiria kwamba kiasi cha watu milioni 2.9 ambao ni sawa na asilimia 27 ya kaya wataendelea kukumbwa na ukosefu wa chakula wakati wa kipindi cha baada ya mavuno, Januari na Machi mwaka 2022.

Katika maeneo ya mijini,hadiwatu milioni 2.4 walitarajiwa kutokuwa na chakula cha kutosha kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa karibuni kwenye maeneo ya mijini mwaka huu wa 2021.

Serikali inasema Zimbabwe mwaka huu imepata mavuno mengi, lakini ukosefu wa chakula katika maeneo ya vijijini unaashiria kuwa mavuno kwa hakika hayakuwa makubwa hivyo.

Waziri wa habari Monica Mutsvangwa amesema uhaba wa chakula nchini humo utamalizika kukiwa na uzalishaji zaidi mashambani katika msimu ujao wa mwaka 2021/2022 ambao unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Ameongeza kusema kwamba serikali itahakikisha kuwa wakulima wana bidhaa za kutosha na fedha wanazohitaji ili kukidhi mahitaji ya wote, binadamu na matumizi ya viwandani.

Zimbabwe iliwahi kuwa mzalisihaji mkubwa wa chakula katika eneo hilo,lakini kwa miaka mingi imekabiliwa na uhaba wa chakula, na kulazimishwa kutegemea misaada ya taasisi za kibinadamu kama World Vision, USAID na WFP ili kuwalisha watu wake.

Serikali inalaumu matatizo ya kutokea ukame wa mara kwa mara, lakini wakosoahi wake wanazungumzia program ya mageuzi ya ardhi iliyokuwa na ovyo sana, ambayo ilianza mwaka 2000 na kywakoseshaz makazi wakulima wa kizungu kutoka kwenye ardhi zao.

XS
SM
MD
LG