Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:11

UN yakabiliwa na changamoto za misaada kwa wakimbizi wa Sudan


Wakimbizi kutoka Sudan wakiwa Metema, baada ya kuvuka kwenda Ethiopia, tarehe 2023. Picha na Amanuel Sileshi/AFP.
Wakimbizi kutoka Sudan wakiwa Metema, baada ya kuvuka kwenda Ethiopia, tarehe 2023. Picha na Amanuel Sileshi/AFP.

Umoja wa Mataifa unajiandaa kwa zaidi ya watu 860,000 waliokimbia mapigano nchini Sudan, wakati nchi jirani ya Chad tayari imeshapokea zaidi ya wakimbizi 30,000.

Makundi ya misaada yanasema yanajitahidi kukabiliana na mmiminiko wa ghafla, yanasema yatalazimika kusitisha kabisa misaada nchini Chad mwezi huu kama hawatapokea ufadhili zaidi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), linasambaza chakula kwenye mpaka wa Chad na Sudan.

Wafanyakazi wa misaada wanasema hali ya wakimbizi nchini Chad ilikuwa mbaya hata kabla ya mzozo wa Sudan kuzuka mwezi uliopita.

WFP inapanga kusitisha misaada yote kwa zaidi ya wakimbizi 700,000 na watu waliokoseshwa makazi nchini Chad mwezi huu kwa sababu ya ukosefu wa fedha, kulingana na ripoti ya Jumanne ya shirika la habari la Reuters.

Mbali na wakimbizi wa hivi karibuni, Chad tayari ilikuwa mwenyeji wa maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan waliokimbia ghasia za miaka mingi katika jimbo jirani la Darfur.

Satahir Mohamed Abdullah ni mwalimu wa somo la Kiingereza kutoka Geneina, Darfur magharibi. Anasema wiki tatu zilizopita, wanaume wenye silaha ambao anaamini wanashirikiana na RSF waliingia mjini kwao wakiwa na farasi, ngamia na pikipiki, walipora na kuchoma moto nyumba pamoja na kuwaua wakazi wa mji huo.

Anasema kuwa mzozo wa kugombania madaraka kati ya kikosi cha RSF na jeshi la Sudan unamaanisha kuwa watu kama hawa sasa wanaweza kufanya lolote bila ya kukhofia kuchukuliwa hatua.
“Kila mtu anataka kuwa rais wa Sudan. Hilo ni tatizo lao, lakini kuna watu wengine. Ni wezi na wako na makamu wa rais. Ukiwa na gari wanaweza kuichukua, ukiwa na bidhaa dukani, wanaweza kuja na kuzichukua. Kama utakataa wanaweza kukuua,” Alisema Abdullah.

Wakimbizi waliovuka mpaka kutoka Sudan kwenda Ethiopia wakiwa na mali zao. Picha na Amanuel Sileshi/AFP.
Wakimbizi waliovuka mpaka kutoka Sudan kwenda Ethiopia wakiwa na mali zao. Picha na Amanuel Sileshi/AFP.

Alikimbia yeye na mke wake na watoto, na kuwasili Koufroune, Chad, ambako yeye na familia yake walipata hifadhi kwenye makazi madogo sana huku joto likiwa kali sana.

Kwa vile sasa yuko hapa, anakabiliwa na tishio jipya.

El Saida Ibrahim Mohammed Adam anasema aliwasili Koufroune akiwa na mtoto wake mgongoni, na safari yake ilikuwa imejaa khofu na hatari.

Alisema anajihisi yuko salama mbali na vikosi vyenye silaha nchini Sudan, angalau, lakini hapa watu wana shida zilizokithiri.

Adam alisema "Hakuna chakula, maji wala mablanketi. Baadhi ya wakimbizi wengine hawana chakula cha kutosha. Familia tisa au kumi zinapaswa kugawana kiwango kidogo cha chakula. Kuna watoto wengi hapa.

Na pia aliongeza “Mama alijifungua mtoto wake na kisha akafariki, hivyo kuna watoto wachanga na wazee, pamoja na wagonjwa na majeruhi. Watoto wengi wanakufa njaa, na hawana hata kitu chochote cha kuvaa. Hawana mahali pa kujikinga na joto la jua au upepo mkali."

Mkurugenzi wa WFP nchini Chad Pierre Honnorat, alisema wakimbizi wanaotoka Sudan wanaongeza shinikizo kwa kile kidogo kilichosalia.

"Inashtua. Ni muhimu. Kwa hiyo, leo, zaidi ya hayo, juu ya uhaba wa chakula ambao umo nchini Chad, sasa kuna wageni wote hao, jambo ambalo linasababisha changamoto kubwa kwa wenyeji,” alisema Honnorat.

XS
SM
MD
LG