Kwa mujibu wa taarifa ya UN kuna watu milioni moja na nusu walioambukizwa na ugojwa huo katika kipindi cha miezi miwili ilyopita.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limeeleza kwamba kumekuwepo na watu milioni milioni 5.7 walioambukizwa na malaria tangu mwanzo wa mwaka 2019 na watu 2,700 kati yao wamepoteza maisha.
Licha ya takwimu hizo serikali ya Bujumbura haijatangaza mlipuko huo kuwa ni janga wala kutoa taarifa yeyote kuhusianana na mlipuko huo.
Hapo mwezi Agosti idara ya huduma za dharura ya UN (OCHA) ilitangaza kwamba malaria imefika kiwango cha janga la kitaifa, lakini wizara ya afya ya Burundi ilipinga takwimu hizo na kutoa takwimu zake ikieleza kwamba ni watu milioni 4.3 ndio walioambukizwa na watu 1,400 ndio walofariki kwa kipindi cha miaka miwili.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC