Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 14:48

UN : Haki za binadamu haziwezi kukamilika bila ya haki za wanawake.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Wanaharakati wa haki za wanawake wanasema licha ya juhudi kubwa zilizochukuliwa kutekeleza na kuimarisha haki za wanawake kote duniani mnamo miongo ya hivi karibuni, bado maendeleo yamekuwa yakipatikana pole pole.

Kuwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wanawake wanaendelea kudharauliwa, kulipwa mishahara ya chini kuliko wanaume, kunyimwa nafasi nzuri za kuendelea mbele pamoja na kuendelea kushuhudia aina mbali mbali za unyanasaji na ghasi kote duniani.

Mashirika ya kimataifa na watetezi wa haki za wanawake wanatoa wito mwaka huu wa kuwepo usawa wa jinsia na kutokomeza hatimae ghasia dhidi ya wanawake na wasichana kote duniani.

Lengo la siku hii

Siku ya kimataifa ya wanawake ilitangazwa kwa lengo la kusherehekea mafanikio ya wanawake katika uchumi, masuala ya kijami na kisiasa. Vile vile UN ilitaka siku hiyo itumike kuhamasisha haki za wanawake ambazo wanaharakati wanasema zingali nyuma bado kama anavyoeleza katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa UN

Katibu Mkuu wa UN anasema : Haki za binadamu haziwezi kukamilika bila ya haki za kibinadamu za wanawake. Na mnamo mwaka huu ambayo inaadhimisha miaka 25 tangu tangazo la Bejing, tumeshuhudia juhudi za kurudisha nyuma haki za wanawake. Hiki kiwango cha kushtusha cha ubaguzi dhidi ya wanawake, mashambulio dhidi ya watetezi wa haki za wanawake, pamoja na kupitisha sheria na sera zinazosababisha uwonevu na kuwateng wanawake."

Mkutano wa Beijing

Mnamo mwaka 1995 mataifa 189 yaliidhinisha tangazo la Bejing lililoandaa ajenda ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya usalama na uchumi wa wanawake. Miongo kadhaa baadae, UN unaripoti kwamba kungali na viwango vya juu vya ghasia, unyanyasji na ubaguzi dhidi ya wanawake. Dk Chantal de Jonge rais wa taasisi ya wanawake katika usalama wa kimataifa, anasema hii yote inatokana na kukosekana kwa wanawake katika nafasi muhimu za madaraka.

Dkt Chantal de Jonge Oudraat, Rais wa taasisi ya wanawake katika usalama wa kimataifa WIIS.

Wanawake wapewe nafasi ya uamuzi

Ni sehemu moja tu ya jamii ambayo imekuwa ikichukua uamuzi kuhusiana na masuala haya. Na ndio maana ni muhimu kuwaweka wanawake kwenye meza ya kufanya maamuzi. Si jambo la ajabu ni lazima tuwaalike. Ni lazima tuwape nafasi ya kupaza sauti zao.

Ripoti ya UN

Hata hivyo Ripoti ya Shirika la UN kwa ajili ya Wanawake, Plan International na UNICEF inaonesha kumekuwepo hata hivyo na maendeleo fulani kwa wanawake na wasichana hasa katika nyaja ya elimu.

Lakini Patty Alleman mtaalamu muandamizi wa masuala ya jinsia na maendeleo kwenye shirika la umoja wa mataifa inyoshughulikia watoto akizungumza kwa Skype anasema maendeleo hayo hayatoshi.

Patty Alleman mtaalamu muandamizi wa masuala ya jinsia na maendeleo, UNICEF anachambua baadhi ya changamoto akisema : "Tunazingatia elimu, hatari za ghasia, tunaangazia suala la hedhi. Kuna mambo mengi na ninadhani ukiangalia kwa ujumla, kwa hakika hakuna nchi yeyote duniani iliyofanikiwa kufikia usawa katika mambo hayo yote.

Ripoti hiyo ina sisitiza kwamba hali katika nchi za kusini mwa janga la Sahara ndio inatia wasi wasi mkubwa zaidi.

Kauli ya UNICEF

Patty Alleman mtaalamu muandamizi wa masuala ya jinsia na maendeleo, UNICEF anasema : "Hebu angalia kiwango cha ndowa za utotoni, kimebadilika kidogo kutoka mtoto mmoja 1 kuolewa kati ya nne kupunguka na kua moja kati ya tano, na nyingi zinatokea Afrika. Hali ni sawa inapohusu wanafunzi kutoka shule ya msingi kuelekea sekondari, tungali tuna idadi ndogo kabisa afrika ya wasichana kubaki shule na kupata maarifa wanayohitaji kufanikiwsa katika maisha yao."

Itahitaji utawala bora kuweza kushughulikia masuala haya anasema balozi aliyestahafu Phillip Carter.

Balozi Phillip Carter Rais wa shirika la Mead Hill anasema : "Huwezi kupuuzi asili miam 50 ya wakazi na kutarajia maendeleo hasa katika upande wa kiuchumi, kijami na Amani."

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG