Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:04

UN yaitaka Kenya isitishe bomoa bomoa Kibera


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) wameitaka Kenya isitishe zoezi la kuwahamisha watu kutoka makazi ya Kibera, mjini Nairobi, Kenya.

Watalaamu hao wametoa kauli Ijumaa kulaani kitendo hicho na kuitaka serikali ya Kenya isitishe zoezi hilo mpaka pale utaratibu wa kisheria na usalama wa kutosha utakapofanyika.

Pia wanasisitiza kwamba serikali ya Kenya ifuate sheria kuhusu njia sahihi za kuwahamisha watu kwa mashauriano na ushirikiano kwa ajili ya maendeleo.

Wataalamu hao wanasema serikali inatakiwa kuendesha zoezi hili kulingana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu kama inavyopendekezwa na kamati za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa zoezi hilo lililanza alfajiri ya tarehe 23 mwezi huu wa Julai.

Zoezi hilo litawaathiri zaidi ya wakazi elfu 30 ambao wataachwa bila makazi. Hadi kufikia Jumamosi tangu operesheni hiyo ilipoanza takriban watoto 2000 wamekuwa hawaendi shuleni.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa bomoa bomoa hiyo imefanyika kinyume na makubaliano ya hapo awali kati ya Mamlaka ya barabara za mijini Kenya Urban Roads Authority ( KURA), Tume ya kitaifa ya ardhi na Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Kenya (KNCHR).

Vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilianzishwa bila ya kutolewa taarifa ya mapema na bila ya kuwepo na mpango wowote wa kuwapatia watu makazi mbadala.

XS
SM
MD
LG