Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:47

Umoja wa Mataifa wafungua mkutano wa Baraza Kuu


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lafungua rasmi mkutano wa kila mwaka

Kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimefunguliwa rasmi leo Jumanne kikiwa na zaidi ya viongozi mia moja wa nchi kujadilia maswala kadha wa kadha ikiwemo swala la taifa huru la Palestina, hali ya baadaye ya Libya baada ya Ghadafi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Swala kuu katika ajenda ya mkutano huo ni uwanachama wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na maswala mengine ya kisiasa. Wiki jana baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lilipiga kura kwa wingi kuunga mkono swala la kukabidhi kiti cha Libya kwa Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC) na hivyo kuashiria kuwa linatambua rasmi kuondoka madarakani kwa Moammar Ghadafi. Rais Barack Obama wa Marekani pia amewasili New York kwa mkutano huo na vikao vingine kando na mkutano huo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Bwana Obama anatazamiwa kukutana na kiongozi wa Baraza la Mpito la Libya Mustafa, Abdel Jalil na rais wa taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini Salva Kiir miongoni mwa wengine .

XS
SM
MD
LG