Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:28

Mataifa mengi yaunga mkono taifa la Palestina


Ukumbi wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Ukumbi wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Maswali ya kutambuliwa taifa la Palestina, wimbi la mageuzi ya kidemokrasia huko Mashariki ya Kati na mzozo wa kiuchumi duniani yaliyochukua nafasi ya juu katika hotuba za viongozi katika kikao cha ufunguzi cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Jumatano mjini New York.

Katibu mkuu Ban ki-Moon alifungua kiako cha 66 cha kila mwaka cha Baraza Kuu, la Umoja wa Mataifa kwa kutoa ripoti ju ya hali ya dunia. Na habari alizoeleza hazikuwa nzuri hivyo, kwani kuna karibu watu bilioni 7 duniani leo wanao n’gan’gnia rasilmali isiyotosha wakikabiliwa pia na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, ajali asili, mapigano na mzozo wa kiuchumi.

“Hizi ni changamoto za kipekee. Hatuwezi kukabiliana nazo kwa njia za kawaida. Tunachohitaji zaidi kuliko kitu kingine kile ni umoja wetu.”

Bw Ban alizungumzia pia suala lililogubika mikutano ya wiki nzima, juhudi ya Wapalestina kuomba uwanachama kamili katika Umoja wa Mataifa.

“Kwa muda mrefu sasa tumekubali kwamba Wapalestina wanastahiki taifa lao. Israel inahitaji usalama. Wote wawili wanataka amani, sisi tuna ahidi juhudi zetu zote kusaidia kufikia amani kupitia suluhisho kwa njia ya majadiliano”.

Kuhusiana na wimbi la mageuzi ya kidemokrasi huko Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, bw Ban alisema imekuwa chanzo cha kuhamasisha wengi. Lakini alikuwa na wasi wasi kutokana na ukandamizaji wa miezi sita unaofanywa na serikali dhidi ya wapinzani huko Syria, akisema ni lazima ghasia hizo zisitishwe na wakati wa kuchukua hatua ni sasa.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alipendekeza kile ambacho ana matumini kitakua mpango utakao tanzua mzozo ulokwama wa Palestina. Alipendekeza Wapalestina wapatiwa hadhi ya taifa lisilo mwanachama kutoka muangalizi kwenye Baraza Kuu, pamoja na kurudi katika mazungumzo ya amani na waisrael.

“Hebu tuwapatiye mwezi mmoja kuanza majadiliamno, miezi sita kufikia makubaliano juu ya mipaka na usalama, mwaka mmoja kufikia makubaliano ya kudumu”.

Rais Barack Obama wa Marekani ambae utawala wake umesema ikilazimika, itatumia kura yake ya turufu kuwazuia Wapalestina kuchukua uwamuzi wa kipekee kutafuta uwanachama wa Umoja wa Mataifa alisema hakuna njia ya kukatiza kufikia amani ikiwa ni pamoja na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia juu ya wimbi la mapinduzi ya nchi za kiarabu na matukio mengine muhimu bw Obama alisema imekuwa mwaka wakukumbukwa.

“Utawala wa Gadafi umeondolewa, Ben Ali na Mubarak hawako tena madarakani. Osama bin laden ametoweka na wazo kwamba mabadiliko yanaweza kupatikana tu kwa ghasia limezikwa nae. Kuna kitu kinachotendeka katika dunia yetu. Jinsi mambo yanafanyika sio namna ilivyokuwa ikifanyika”.

Na ishara nyingine ya mambo mazuri ni kwamba kwa mara ya kwanza mkutano wa mwaka ulifunguliwa na mkuu wa taifa mwanamke, rais wa Brazil Dilma Rousseff. Mara moja akatangaza kwamba hii ni karne ya wanawake.

XS
SM
MD
LG