Jeshi la Ukraine lilisema majeshi yake ya angani yalitungua makombora sita aina ya Kalibr, pamoja na ndege zisizo na rubani 21, zilizokuwa zikipaa katika anga ya Odesa, lakini vifusi kutokana na milipuko hiyo, ndivyo vilivyosababisha uharibifu ardhini.
Ukraine ilisema pia ilitungua ndege zisizo na rubani katika eneo la Mykolaiv, kusini mwa nchi hiyo, huku jeshi likikamata jumla ya ndege 31, zisizo na rubani, kati ya 36 kote nchini.
Eneo la Odesa ni kitovu cha bandari nyingi ambazo zilikuwa sehemu ya Mpango wa Nafaka wa Bahari ya Black Sea, uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki, ili kuwezesha usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine, kwenda kwenye soko la kimataifa.
Russia ilisema Jumatatu kwamba inasitisha ushiriki wake katika makubaliano, yaliyowezesha usafirishaji wa bidhaa kwa usalama, kupitia bandari za black sea, wakati vita kati yake na Ukraine vikiendelea.
Forum