Zelenskiy alisema katika ujumbe wake wa kila usiku kwa njia ya video kwamba Ukraine ni chanzo cha chakula kwa watu milioni 400.
“Afrika ina haki kwa utulivu, Asia ina haki kwa utulivu,” alisema.
Russia Jumatatu ilisitisha ushiriki wake katika makubaliano hayo ya mwaka mmoja ambayo yanaruhusu Ukraine kuuza nje nafaka kupitia njia salama ya usafirishaji katika bahari ya Black Sea, na kusababisha wasiwasi katika nchi maskini kwamba bei zitapanda na kufanya iwe vigumu kuzimudu.
Moscow ilipendekeza kwamba ikiwa matakwa ya kuboresha mauzo ya nje ya nafaka na mbolea yake yatatekelezwa, itafikiria kufufua tena makubaliano hayo yanayojulikana kama mpango wa nafaka wa Black Sea.
Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki yalisifiwa kuwa yalizuia mzozo wa chakula duniani kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine mwezi Februari 2022 na kufungwa kwa bandari za Black Sea.
“Ukraine, Umoja wa Mataifa na Uturuki kwa pamoja wanaweza kuhakikisha shughuli kwenye njia salama ya chakula na ukaguzi wa meli. Hii ni muhimu kwa ulimwengu mzima, Zelenskiy alisema.
Forum