Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 23:50

Ukraine yaanza kusambaza chakula, maji na dawa Kherson baada ya Russia kuukimbia mji huo


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiondoka katika hafla fupi ya kupandisha bendera ya Ukraine katikati ya mji wa Kherson, Ukraine.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiondoka katika hafla fupi ya kupandisha bendera ya Ukraine katikati ya mji wa Kherson, Ukraine.

Maafisa wa Ukraine Jumapili walianza kupeleka chakula, maji na dawa katika mji wa kusini wa  Kherson, siku mbili baada ya majeshi ya Kyiv kuingia katika mji mkuu wa mkoa wa kimkakati ambao ulikuwa umetekwa na Russia mara baada ya vita kuanza na hivi sasa wameukimbia.

Zaidi ya robo tatu ya wakazi 300,000 wa Kherson wameukimbia mji huo, wakiwaacha nyuma watu 75,000 kuishi chini ya uvamizi wa Russia kabla ya majeshi ya Moscow kuondoka wiki iliyopita na majeshi ya Ukraine kuanza kuchukua udhibit.

“Majeshi ya uvamizi ya Russia na washirika wake walifanya kila wawezalo kuwapa madhila kadiri ilivyowezekana watu waliokuwa katika mji huo katika kipindi hiki cha mpito, wiki kadhaa za kusubiri, miezi kadhaa,” mshauri wa meya wa Kherson, Roman Golovnya, alisema kupitia televisheni ya taifa.

Majeshi ya Ukraine yakiendesha moja ya vifaru vya Russia vilivyokamatwa huko Kherson, Ukraine, Jumapili, Nov. 13, 2022.
Majeshi ya Ukraine yakiendesha moja ya vifaru vya Russia vilivyokamatwa huko Kherson, Ukraine, Jumapili, Nov. 13, 2022.

Majeshi ya Ukraine walihofia kuwa majengo mengi katika eneo kubwa la Kherson yangekuwa yameharibiwa vibaya sana, kama ilivyokuwa katika miji mingine, kama vile Mariupol, lakini wameyakuta kwa sehemu kubwa yako salama, lakini hayana maji ya kutosha. Ukiwa umekombolewa, wakazi wengi wa Kherson walikusanyika mitaani katika siku kadhaa za mwisho, wakipeperusha bendera za Ukraine zenye rangi ya blu na manjano kuonyesha furaha yao.

Wakazi walisimulia habari za mabomu yaliyopigwa na Russia katika mji huo lakini vile vile walisema uwezo wa Ukraine wa kutumia mfumo wa makombora ya viwango vya juu yaliyotolewa na washirika wa Magharibi, ikiwemo Marekani, unaelekea ulivuruga njia kuu za usambazaji mahitaji yaliyokuwa yanapelekwa na Moscow na upangaji wa wanajeshi wao. Wanasema Ukraine waliweza kupiga maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na Russia a kwa msaada wa mtandao wa majasusi.

Pia, wakazi wa Kherson walieleza kuhusu marafiki zao na wanafamilia ambao walikamatwa na majeshi ya Russia na walikuwa hawajulikani waliko kwa zaidi ya miezi tisa ya uvamizi huo wa Russia.

Hali kadhalika maisha bado hayajarejea kuwa ya kawaida.


XS
SM
MD
LG