Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 22:25

Wanajeshi wa Russia wamekufa maji wakikimbia na wengine kuamua kuvaa sare za kiraia wasitambuliwe


Mkaazi wa Kherson akisherekea kuingia kwa wanajeshi wa Ukraine mjini humo baada ya wanajeshi wa Russia kuondoka Nov 11, 2022
Mkaazi wa Kherson akisherekea kuingia kwa wanajeshi wa Ukraine mjini humo baada ya wanajeshi wa Russia kuondoka Nov 11, 2022

Wakaazi wa Kherson wamesherekea kuingia kwa wanajeshi wa Ukraine mjini humo na kuondoka kwa wanajeshi wa Russia.

Russia imeondoka Kherson, mji mkubwa pekee ambao wanajeshi wake walikuwa wameshikilia tangu walipovamia Ukraine mwezi Februari.

“Leo ni siku ya historia. Tunarejesha sehemu ya kusini ya nchi yetu, tunarejesha Kherson,” amesema rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy katika ujumbe wa video, akiongezea kwamba “kwa sasa, wanajeshi wetu wapo nje yam ji huo na karibu tunaingia katikati ya mji, lakini wanajeshi maalum tayari wameingia mjini.”

Russia imesema kwamba imeondoa wanajeshi wake 30,000 kutoka sehemu iliyo karibu na mto Dnipro, bila kupoteza mwanajeshi yeyote.

Lakini Ukraine imetoa taaswira ya wanajeshi wa Russia wakikimbia sehemu hiyo kwa haraka sana na hata kuacha nyuma sare zao, silaha na wengine kufa maji wakijaribu kujiokoa.

Wanajeshi wengine wa Russia wanaripotiwa kuvaa sare za kiraia waliposhindwa kuvuka mto Dnipro wakati wanaondoka Kherson.

Kuondoka kwa wanajeshi wa Russia katika mji wa Kherson ni mara ya tatu wanajeshi hao kuripoti kujiondoa katika ngome walizokuwa wanashikiliwa katika vita walivyoanzisha nchini Ukraine.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba mji wa Kherson umerejeshwa chini ya udhibithi wa Ukraine na kutaka wanajeshi wa Russia waliosalia mjini humo kujisalimisha kwa wanajeshi wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG