Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:32

Ukraine haifikiri kutafuta suluhu na Russia


Rais wa RussiaVladimir Putin (kushoto) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.
Rais wa RussiaVladimir Putin (kushoto) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Mwendesha Mashtaka  Mkuu wa Ukraine amesema nchi yake haifikirii kufanya mashauriano na Russia katika kumaliza  uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.

Katika mahojiano na shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, mjini Kyiv, Andriy Kostin alisema Moscow lazima iwajibishwe kwa uvamizi wake nchini Ukraine.

Kostin, ambaye anataka kufungua mahakama maalum ya kimataifa ya uhalifu, alisema anataka fidia itakayopatikana kupitia kukamatwa kwa mali za Russia.

FILE - Andriy Kostin
FILE - Andriy Kostin

Alitofautiana na dhana ya kuwa watu ulimwenguni wanapata tabu kwa sababu ya Ukraine. “Watu hao hawasikii makombora. Hawajui nini maana ya nchi kupigwa mabomu,” alisema. “Hawajui nini mauaji, ubakaji na wizi wa ngawira.”

Wakati mwendesha mashtaka huyo anakubaliana na watu wa Ulaya kuwa wanalipa zaidi kwa chakula na mafuta tangu uvamizi huo, alisema Waukraine “wanalipa gharama ya maisha yao.”

Kostin alisema ushahidi wa mateso na mauaji holela unajitokeza “katika kila kijiji na kila mji,” ikiwa pia ushahidi wa manyanyaso ya kingono d wanawake na watoto.

XS
SM
MD
LG