Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:29

Russia imeondoa wanajeshi wake Kherson kufuatia mashambulizi ya Ukraine


Wanajeshi wa Ukraine wakirusha makombora kuelekea ngome za wanajeshi wa Russia mashariki mwa Donetsk Okt. 23, 2022
Wanajeshi wa Ukraine wakirusha makombora kuelekea ngome za wanajeshi wa Russia mashariki mwa Donetsk Okt. 23, 2022

Russia imewaamuru wanajeshi wake waondoke kutoka mji wa Kherson, mji mkuu pekee ambao umekuwa chini ya udhibiti wa Moscow tangu wanajeshi wa Russia walipoivamia Ukraine, Februari mwaka huu.

Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, amesema kwamba aliamuru kuondoka kwa wanajeshi hao kutoka mji wa Kherson kusini mwa Ukraine kufuatia mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine.

Kamanda wa wanajeshi wa Russia amesema kwamba haiwezekani kutuma wanajeshi katika mji wa Kherson.

Kuondoka kwa wanajeshi hao ni pigo kubwa sana kwa Russia, tangu kujitangazia kujiingiza sehemu hiyo.

Tangazo la Russia pia linajiri wakati kuna ripoti kwamba Kirill Stremousov, afisa wa Russia ailiyeteuliwa na Moscow kuliongoza eneo la Kherson, amefariki kutokana na ajali ya barabarani. Alikuwa ndani ya gari lake.

Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, amesema kwamba ni mapema sana kuzungumzia hatua ya wanajeshi wa Russia kuondoka Kherson.

“Hadi wakati bendera ya Ukraine itakapopepea Kherson, ndipo tutaweza kuzungumzia kwa kina hatua ya Russia kuondoka.” Amesema Podolyak, akiongezea kwamba “Ukraine haiwezi kuzichulkuia hizi taarifa kwa uzito.”

XS
SM
MD
LG