Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:49

Marekani 'inataka Ukraine kufanya mazungumzo na Russia’


Rais wa Ukraine Zelenskiy akizungumza na rais wa Marekani Joe Biden kwa njia ya simu, Kyiv Okt 4, 2022
Rais wa Ukraine Zelenskiy akizungumza na rais wa Marekani Joe Biden kwa njia ya simu, Kyiv Okt 4, 2022

Marekani inataka Ukraine kuweka ishara za kutaka kuanzisha mazungumzo ya amani na Russia.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, ambalo limenukuu gazeti la Washington Post, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kwamba Russia inaendelea kuongeza kasi ya vita na haionyeshi dalili za kufanya mazungumzo ya amani.

Gazeti la Washington Post linasema kwamba maafisa wa Marekani hawaishinkizi Ukraine kufanya mazungumzo na Russia, lakini ni jaribio la kimkakati kuhakikisha kwamba Ukraine inaendelea kuungwa mkono na mataifa mengine.

Maafisa wa Ukraine na Marekani wamekiri kwamba hatua ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kukataa kufanya mazungumzo na rais wa Russia Vladimir Putin, imepekelea hali ya wasiwasi katika baadhi ya mataifa ya Ulaya, Afrika na Amerika ya Kusini, ambapo athari za vita hivyo vimepelekea kuongezeka kwa gharama ya maisha, ukosefu wa chakula na mafuta.

Zelenskyy alisaini amri ya kiutendaji Oktoba 4 na kutangaza rasmi kutokuwepo nafasi ya kufanyika mazungumzo na Putin, lakini akasema yupo huru kufanya mazungumzo hayo na Russia.

Baraza la Usalama wa taifa huko White house, halijatoa taarifa yoyote kuhusu ukweli uliomo kwenye ripoti hiyo ya gazeti la Washington Post.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kwamba “tumesema na tutaendelea kusema kwamba vitendo vina ujumbe mzito kuliko maneno. Iwapo Russia ipo tayari kwa mazungumzo, lazima iache kuishambulia Ukraine kwa mabomu na makombora, na iondoe wanajeshi wake nchini Ukraine.”

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesisitiza ujumbe wa rais wa Ukraine alioutoa Ijumaa kwamba "tupo tayari kwa amani, na tumesema hili mara kadhaa.”

Katika hotuba yake kwa taifa Ijumaa, Zelenskyy alisema kwamba “dunia inajua msimamo wetu. Kuheshimu kanuni za Umoja wa Mataifa, kuheshimu mpaka wetu, kuheshimu watu wetu.”

Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan, alisema Ijumaa wakati wa ziara yake nchini Ukraine kwamba Marekani itaendelea kutoa msaada kwa Ukraine hata baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula, utakaofanyika Jumanne Novemba 8.

XS
SM
MD
LG