Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:23

White House: "Trump Anaheshimu Uhuru wa Habari, Lakini ni Jukumu la Pande Zote Mbili"


Sean Spicer akizungumza na waandishi
Sean Spicer akizungumza na waandishi

Msemaji wa White House Sean Spicer amemtetea Rais Donald Trump Jumanne kwa kuviita vyombo vya habari “adui wa wananchi wa Marekani” na kuvishutumu baadhi ya vyombo hivyo kwa kuripoti habari za upande moja na zisizo za kweli.

Spicer amewahakikishia waandishi wa habari White House kwamba rais anaheshimu kwa dhati kabisa kifungu cha uhuru wa kujieleza kilichopo katika katiba ya Marekani. Lakini amesema hilo ni wajibu kutekelezwa na pande zote mbili.

“Nafikiri rais anaelewa kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimeenda kinyume kwa kutotoa taarifa sahihi na za haki katika kuripoti mambo yanayojiri nchini,” Spicer amesema.

Msemaji wa White House aligusia baadhi ya malalamiko ya Trump kuhusu vyombo vya habari akijibu swali la mwandishi, alotaka kujua iwapo rais “ana majuto yoyote juu ya kauli yake au ufafanuzi katika shutuma” dhidi ya vyombo vya habari kwa kuwaita “maadui,” wakati wa mkutano mrefu na waandishi Alhamisi iliyopita.

Hata hivyo Spicer hakutoa mifano yoyote ya habari zinazodaiwa kuwa sio sahihi au sisizo tenda haki katika repoti hizo.

Pia aliulizwa kuhusu habari juu ya Trump kwamba hakuwa mwangalifu katika kushughulikia taarifa za siri wiki iliyopita, wakati alipofahamishwa kuhusu jaribio la kombora lililofanywa na Korea Kaskazini alipokuwa katika chakula cha usiku kwenye Jumba lake la Mar-a-Lago resort huko Florida.

Ilidaiwa kuwa watu wengine waliokuwa kwenye chakula wakati huo waliona maafisa wa juu wameizunguka meza ya Trump wakishauriana juu ya makaratasi na wakipiga simu.

Ilivyokuwa watu wanakula kwa kutumia mwanga wa mishumaa katika meza hizo, washauri wa Trump wakawasha tochi za simu ilikumurika makaratasi. Mtu moja aliyekuwa kwenye ukumbi huo wa chakula alipiga picha hiyo ya tukio lisilo la kawaida na kuposti kwenye mitandao ya jamii.

Baada ya tukio hilo kuonekana kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya taarifa za vyombo vya habari vilikuwa vikishabikia kuwa rais na wasaidizi wake walikuwa hawajatumia busara katika kushughulika taarifa za siri na nyeti mbele ya watu waliokuwa wanaona kitendo hicho, ambao hawahusiani na White House. Spicer alikanusha habari hizo Jumanne.

Inashangaza vipi habari kama hizi zilienezwa,” msemaji wa White House amesema.

“Picha inatumwa kwenye mitandao, rais anaonyeshwa akiwa na kipande cha karatasi, na mara watu wanatoa hukumu ni lazima anazungumzia habari za siri hadharani.”

XS
SM
MD
LG