Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:13

Wizara ya Usalama wa Ndani Yatoa Agizo Kuhusu Wahamiaji


Waziri wa Usalama wa Ndani John Kelly
Waziri wa Usalama wa Ndani John Kelly

Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani imetoa nyaraka mbili mpya zikielezea jinsi ya kutekeleza amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump.

Nyaraka hizo zilizotolewa Jumanne na Waziri wa wizara hiyo, John Kelly, ni katika juhudi za kuzuia wahamiaji haramu, wakati huo huo wakichukua hatua kuwaondoa wahamiaji wasiokuwa na vibali vya kuishi Marekani.

Pia nyaraka zimeainisha orodha ya vipaumbele; kwa wahamiaji ambao wanatikiwa kuondolewa mara moja, zinatoa muhtasari wa mpango wa kuwaajiri maelefu ya watekelezaji wa amri hiyo ya utendaji, na kuvipa uwezo vyombo vya serikali kutekeleza kazi za uhamiaji na kutumia sheria zilizopo.

“Agizo hili lianze kutumika mara moja,” waraka umeeleza, “ idara za utumishi zitatekeleza kwa uaminifu sheria za uhamiaji za Marekani kwa kuwashughulikia wageni wote wanaostahili kuondolewa.”

Nyaraka hizo, ambazo zilivuja siku ya Ijumaa kwa vyombo vya habari, zinatofauti moja tu na amri ya kiutendaji iliyotolewa awali: Nalo ni programu ya DACA inayotaka kuahirisha kuchukua hatua kwa watoto waliopokelewa Marekani wakiwa wadogo.

Takriban watu wasio na vibali 750,000 ambao waliletwa Marekani wakiwa watoto—wanaojulikana kama “dreamers” --- wanategemea programu hiyo kuishi na kufanya kazi Marekani bila ya hofu ya kuondolewa.

Trump aliviambia vyombo vya habari wiki iliyopita ana mpango wa kushughulikia vijana walio chini ya programu ya DACA kwa “huruma,” jambo aliloliita “ni gumu mno.”

“Wapo vijana ambao ni hodari sana, naweza kusema wengi wao,” Trump amesema. “Ninapata ugumu sana kufanya kile ambacho sheria inataka nifanye hasa, na mnajua sheria ni kali.”

Nyaraka zilizotolewa Jumanne ni tafsiri ya moja kwa moja ya amri ya kiutendaji ya uhamiaji iliyokuwa imesainiwa na Trump Januari 25.

XS
SM
MD
LG