Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:09

Uhuru, Raila hawatabadilisha wasimamizi wa uchaguzi katika kambi zao


Raila Odinga na Uhuru Kenyatta
Raila Odinga na Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta na hasimu wake wa kisiasa Raila Odinga wanaendelea kuwatumia makamanda wao walioshiriki kusimamia uchaguzi wa mwezi August 2017 katika kinyang’anyiro cha urais unaorudiwa tena nchini Kenya.

Hata hivyo wanawashirikisha wataalamu wa IT, hatua ambayo imeelezwa imetokana na jinsi teknolojia ilivyokuwa imechangia kuathiri matokeo ya uchaguzi wa August 8; matokeo ambayo yalisababisha kubatilishwa uchaguzi huo na Mahakama ya Juu ya Kenya.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vinasema kufuatia umuhimu wa Teknohama (ICT) katika kuendesha uchaguzi, kambi zote mbili zinashindana katika kupata watu wajuzi au makampuni mahiri katika fani hiyo.

Hatua hiyo ni ya kimkakati ili kuhakikisha kuwa hawasalitiwi na vitendo vyovyote vya udukuzi wa seva zao na mifumo yao ya uchaguzi kama ilivyokuwa imebainika kutokea wakati wa uchaguzi wa August 8.

Uchaguzi wa urais nchini Kenya utarudiwa Octoba 17, kama ilivyokuwa imetangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Katika tamko lake, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati amesema hakutakuwa na uteuzi mpya katika uchaguzi huu.

Chebukati amesema Kiongozi wa NASA peke yake Raila Odinga, na Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na wagombea wenza wao watashiriki.

Mgombea mwenza wa Odinga ni Kalonzo Musyoka na yule wa Kenyatta ni makamu wake William Ruto.

“Tume hiyo inapitia taratibu na hatua zinazohitajika kuendesha uchaguzi huo upya na itawajulisha wadau wote mapema baadae,” amesema

XS
SM
MD
LG