Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:01

Marekani yatoa zaidi ya $840 milioni kuboresha hali ya maisha Uganda


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Serikali ya Marekani imetoa dola milioni 840.4 (Shs 2.9 trilioni) kuboresha afya, sheria, elimu, utulivu wa kisiasa na kuboresha hali za maisha za wananchi wa Uganda.

Taarifa hii iko katika ripoti ya kurasa 55 “Ripoti kwa Watu wa Uganda”, ambayo imetolewa na Ubalozi wa Marekani mjini Kampala wiki hii ikisema kuwa msaada huu ulikuwa kati ya Octoba mwaka jana na September Mwaka huu .

Sekta ya afya Uganda ni yenye kunufaika zaidi na msaada huu uliotolewa, ikiwa imepokea takriban dola milioni 488.3 au Shs 1.7 trilioni zilizotolewa kati ya Oktoba mwaka jana na Septemba mwaka huu. Msaada huu unafanya Marekani kuwa nchi pekee yenye mchango mkubwa wa msaada wa afya nchini Uganda.

Kwa kutenga msaada zaidi katika sekta ya afya, serikali ya Marekani imesema kuwa inadhamiria kupunguza tishio la maambukizi ya maradhi kama vile HIV, kifua kikuu na malaria, ilikuboresha afya za kina mama na watoto wanaozaliwa.

Ripoti hiyo imeelezea kuwa miradi hiyo inayofadhiliwa na Marekani katika sekta hiyo inawapatia madawa ya kuokoa maisha, kuwawezesha watoto wa kike, kuwaokoa kina mama, na kuwapa fursa wananchi wa Uganda kuishi maisha marefu, yenye mafanikio zaidi.

Marekani inaamini kuwa utulivu na amani nchini Uganda ni muhimu katika shughuli zake nchini Uganda na hili pengine linaelezea kwa nini ni nchi ya pili katika kipaumbele cha misaada. Mwaka wa fedha uliopita, Marekani ilitumia dola milioni 279.6 au Shs 951.2 bilioni kwa ajili ya kuimarisha utulivu nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG