Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 12:22

Ufaransa yasaidia juhudi za Marekani kutafuta suluhu Mashariki ya Kati


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson akutana na Mtawala wa Qatar, Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani Doha, Qatar.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson ameondoka Qatar Alhamisi akiwa amefikia mafanikio madogo ya kidiplomasia katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kidiplomasia uliopo kati ya Doha na nchi nne za Kiarabu.

Tillerson alikataa kujibu maswali baada ya mkutano wake wa mwisho katika ziara yake Mashariki ya Kati na Mtawala wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, kabla ya kuondoka kuelekea Washington.

Wakati Tillerson hakuweza kupata ufumbuzi kuhusu mgogoro huo, Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Yves Le Drian anaelekea Mashariki ya Kati kuanzisha mazungumzo upya.

Kwa zaidi ya siku nne, Tillerson amekuwa akizunguka baina ya Qatar, Saudi Arabia na Kuwait katika juhudi za kusuluhisha mgogoro uliokuwepo kati yao.

Alipata makubaliano na Qatar katika kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi, lakini Saudi Arabia, Misri, Bahrain, na Umoja wa Falme za Kiarabu zimesema kuwa hilo halitoshelezi na kuendelea kuitaka Qatar ikubaliane na msharti yao 13 waliotoa.

Doha imetupilia mbali madai hayo, ikisema yanakandamiza uhuru wake. Kati ya masharti hayo ni kuitaka kufunga mtandao wake wa Al Jazeera, kusitisha mafungamano yake na makundi ya Kiislam kama vile Muslim Brotherhood, kuacha mahusiano yake na Iran na kuyaondosha majeshi ya Uturuki katika eneo lake.
Tillerson alizungumza na viongozi wa Qatar baada ya kutumia muda wake Jumatano katika mji wa Saudi ulioko katika pwani ya Red Sea, Jeddah ambako alikutana na wana diplomasia kutoka Saudia Arabia, Misri, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia ulivunja mahusiano ya kidiplomasia na Qatar mapema mwezi uliopita, ukiishutumu Doha kwa kufadhili ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kuwa na ukaribu na mpinzani wao mkubwa Iran. Qatar imetupilia mbali madai yao hayo.

Marekani ina wasiwasi kwamba mgogoro huu unaweza kuyaathiri majeshi yake na operesheni za kupambana na ugaidi na kupelekea Iran kuwa na nguvu kubwa katika eneo hilo.

Qatar imetoa kituo chake cha kijeshi cha al-Udeid kwa Marekani ambacho ni kituo kikubwa katika Mashariki ya Kati na kina ratibu vita dhidi ya Kikundi cha Islamic State huko Iraq na Syria.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG