Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 17:24

Marekani, Qatar zakubaliana kupambana na ugaidi GCC


Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani (R) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson

Marekani na Qatar zimesaini makubaliano juu ya kupambana na ugaidi katika nchi za Ghuba ya Uajemi (GCC).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Jumanne wakati wa ziara yake kwenye mji mkuu, Doha kwamba makubaliano yamefikiwa baada ya wiki kadhaa za mazungumzo ya kiina.

“Mkataba huo unaweka wazi hatua mbalimbali ambazo nchi hizo mbili zitachukua katika miezi ijayo na miaka ya usoni kuingilia kati na kuondoa njia zote zinazofadhili ugaidi na kushinikiza mapambano dhidi ya ugaidi duniani,” Tillerson amewaambia waandishi baada ya kusiani makubaliano hayo.

Tillerson alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Sheikh Mohammad al-Thani katika mji mkuu huo ili kuzungumzia maazimio yanayohusu ugomvi unaohusu Qatar na nchi nyingine nne za Mashariki ya Kati.

Mwezi uliopita, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Misri na wengine walikata mahusiano ya kidiplomasia na kuanzisha vikwazo vya ardhini, baharini na angani dhidi ya Qatar, wakiishutumu nchi hiyo kuwa inasaidia ugaidi.

Ratiba ya Tillerson inahusisha kukamilisha kituo chake cha mwisho katika ziara yake huko Saudi Arabia siku Alhamisi

Mshauri wake wa mawasiliano wa ngazi ya juu R. C. Hammond amesema sababu ya ziara yake ni kutafuta njia yoyote itakayo wezesha kutatua mgogoro huu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG