Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:15

Ufaransa yaanza kutekeleza sheria inayopiga marufuku vazi la abaya mashuleni


Msichana akiwa amevaa abaya akiongea na wenzake huko Nantes, Agosti 31, 2023. Picha na LOIC VENANCE / AFP.
Msichana akiwa amevaa abaya akiongea na wenzake huko Nantes, Agosti 31, 2023. Picha na LOIC VENANCE / AFP.

Mamlaka nchini Ufaransa Jumatatu imeanza utekelezaji wa marufuku mpya wa vazi la abaya mashuleni iliyotangazwa hivi karibuni. Vazi ambalo linavaliwa na wanafunzi wa kiislamu, wakati zaidi ya taasisi 500 zinafanyiwa uchunguzi wakati huu watoto wakirudi mashuleni.

Serikali ilitangaza mwezi uliopita kuwa imepiga marufuku uvaaji wa abaya mashuleni, ikisema kuwa vazi hilo linakiuka kanuni za kutohusisha dini katika elimu ambalo tayari linaonekana kuwa ni vazi la kiislamu ambalo lilishapigwa marufuku kwa madai linaonyesha ufuasi wa kidini.

Hatua hiyo iimewafurahisha wale wenye siasa za mrengo wa kulia lakini wale wa mrengo mkali wa kushoto walidai kuwa inawakilisha dharau za uhuru wa raia.

"Mambo yanakwenda vizuri asubuhi ya leo. Hakuna tukio lolote kwa sasa, tutaendelea kuwa macho siku nzima ili wanafunzi waelewe maana ya kanuni hii," alisema Waziri Mkuu Elisabeth Borne alipoitembelea shule moja iliyoko kaskazini mwa Ufaransa.

Lakini aliongeza kuwa kulikuwa na "baadhi" ya shule ambazo wasichana waliwasili wakiwa wamevaa abaya.

Kuna takriban shule 45,000 na wanafunzi milioni 12 nchini Ufaransa wanaorejea mashuleni Jumatatu.

Sheria hii iliyoanzishwa Machi 2004 ilipiga marufuku "kuvaa mavazi yenye ishara au yanayoashiria ufuasi wa kidini wa wanafunzi " shuleni.

Hii inajumuisha misalaba mikubwa, kippa za Kiyahudi na hijabu za Kiislamu.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari AFP

Forum

XS
SM
MD
LG