Maandamano yameikumba Iran tangu kifo cha Septemba 16 cha Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22, baada ya kukamatwa mjini Tehran kwa madai ya kukiuka sheria kali za jamhuri ya Kiislamu ya mavazi kwa wanawake.
Shirika la habari la Fars lilimnukuu afisa mkuu wa polisi ambaye alisema kanuni hiyo mpya ya programu ya Nazer inaendelea nchini kote.
Mpango wa Nazer, uliozinduliwa mwaka 2020, ulikuwa na wasi wasi wa kkutovaa hijabu ndani ya magari. Ilipozinduliwa mwaka 2020, wamiliki wa magari walituiwa ujumbe mfupi wa maandishi kuwaarifu kuhusu ukiukaji wa kanuni za mavazi kwenye magari.